Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amesema amewataka wanawake mkoani humo kuhakikisha malezi bora na yenye maadili kwa watoto.
Bi. Mrindoko ametoa rai hiyo wakatai wa maadhimisho ya siku ya wanawake yaliyofanyika kimkoa wilayani Mlele ambapo amewaeleza kuwa wasijisahau katika shughuli zao za kuingiza kipato ali watenge muda wa kuzungumza na watoto.
Aidha amesema serikali imeendelea kuboresha huduma mbalimbali za jamii ikiwemo elimu, afya, nishati safi na umeme sambamba na kutoa fursa sawa katika ngazi mbalimbali za maamuzi.
Pia serikali imekuwa ikitoa mafunzo ya ujasiriliamali na mikopo, kutambua makundi ya wanawake na kuwezesha bidhaa zao kutambulika ndani na nje ya nchi.
“Tangu mh. Rais Samia Suluhu Hassan ameingia madarakani vikiundi 666 vya wanawake vimepokea kiasi cha shilingi bilioni 4.3”.
Katibu Msaidizi Jukwaa la wanawake mkoani Katavi Hadija Kapinga akitokea salamu ameshukuru kwa mikopo ya asilimia 10 wanayopata ambayo imewasaidia wanawake kupata na kuinua mitaji yao.
Salamu za wabunge zilizotolewa na mh. Janeth Pinda mbunge wa vitu maalum mkoa wa Katavi amempongeza mh. Rais kwa kumtua.mama ndoo kichwani na kuongeza kuwa sasa suala la bima ya afya kwa wote litakwenda kutatua matatizo ya matibabu kwa wanawake.
Aidha amempongeza Mkuu wa mkoa wa Katavi kwa kupambania suala la uchumi.
Pia amesisitiza kuwa kinamama washirikiane katika malezi ili kuwakinga watoto dhidi ya vitendo vya unyanyasaji.
Aidha wameomba elimu ya sheria iendelee kutolewa kwa wanawake ili waone umuhimu wa kumiliki ardhi na mali za familia.
Awali Afisa Maendeleo ya Jamii Anna Shumbi amesema shughuli mbalimbali zimefanyika katika wiki hii ya wanawake yakiwemo makongamano, utoaji misaada, matendo ya huruma, upandaji wa miti, na utoaji wa vifaa vya kujifungua.kufanya usafi.
