Na. Meleka Kulwa- Fullshangwe Blog, Dodoma
Benki ya Ushirika Tanzania (Coop Bank) imezindua Akaunti ya JUHUDI, bidhaa mpya ya amana ya muda yenye riba ya hadi asilimia 13.5 kwa mwaka. Kupitia kampeni ya miezi mitatu kuanzia Februari 24 hadi Mei 31, 2026,
akizungumza na Waandishi wa Habari Februari 24,2025, Jijini Dodoma, Mkuu wa Idara ya Biashara na Ushirika katika Benki ya Ushirika Tanzania, Bw. Yahya Kiyabo, amesema kuwa benki inalenga kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 300 ili kuimarisha mikopo kwa wajasiriamali wadogo na wa kati. Kiwango cha chini cha kuweka ni shilingi 500,000.aidha, amebainisha kuwa akaunti hiyo inalenga kuimarisha utamaduni wa akiba na kukuza uchumi jumuishi nchini.
Aidha, Mkuu wa Kitengo cha Hazina, Hakim Sheikh, alieleza kuwa si lazima uwe na entries za mwaka mzima. “Kama una mpango wa kuchukua fedha zako baada ya miezi mitatu, unaweza kuweka kwa kipindi hicho tu, na tutakupa entries zako hapohapo. Baada ya miezi mitatu utaweza kuchukua mtaji wako uliowekeza,” amesema
Aliongeza kuwa uamuzi huo umetokana na maombi ya wateja wengi sokoni. “Tumechukua maoni ya wateja wetu na tumeamua kuanzisha bidhaa hii ili kukidhi mahitaji yao, hasa wale wanaotaka mipango ya uwekezaji inayolingana na muda wao,” amesema





