Na Mwandishi wetu, Arusha
WAANDISHI wa habari 140 wa Tanzania watajengewa uwezo wa WAANDISHI WA HABARI 140 KUJENGEWA UWEZO habari za mazingira kupitia kanda mbalimbali nchini.
Mkurugenzi wa shirika la waandishi wa habari la kusaidia jamii za asili (MAIPAC) Mussa Juma ameeleza kwamba waandishi hao watajengewa uwezo kupitia mtandao wa watetezi wa haki za binadamu (THRDC) kwa uwezeshaji wa shirika la umoja wa mataifa UNESCO.
Mussa amesema awali wameanza kutoa mafunzo hayo jijini Arusha kwa waandishi wa habari wa mikoa ya kanda ya Kaskazini na kanda ya kati.
Amesema waandishi wa habari wa mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Manyara, Singida na Dodoma wamepatiwa mafunzo hayo
“Waandishi 140 watajengewa uwezo kwani baada ya kanda ya kaskazini, watafuata waandishi wa kanda ya ziwa, pwani na Zanzibar,” amesema Mussa.
Amesema waandishi hao watajengewa uwezo wa kuandika habari mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi, athari za mazingira katika migodi na uchafuzi wa mazingira kwenye bahari,” amesema Mussa.
Mkurugenzi wa mipango na uendeshaji wa THRDC, wakili Halima Sonda amesema pia waandishi hao watetezi wa haki za binadamu watajengewa uwezo zaidi wa zana za kuimarisha ujuzi na silaha kubwa za uwajibikaji.
Sonda amesema kupitia mafunzo haya waandishi wa habari watajengewa uwezo zaidi wa kuandika habari za mazingira kwenye maeneo mbalimbali.
Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari wa mkoa wa Arusha (APC) Claud Gwandu amesema waandishi wa habari wanapaswa kuandika kwa uzito mkubwa shughuli za kibinadamu kuingilia mapito ya wanyamapori (shoroba).
“Hifadhi ya Taifa ya Tarangire ilikuwa inasifika kwa tembo wakubwa kutokana na mwingiliano wao kupitia ushoroba ila hivi sasa maeneo yao ya mapito nyumba zimejengwa, vituo vya mafuta, tuandikie haya ili yakomeshwe,” amesema Gwandu.
Mmoja kati ya waandishi wa habari waliopata mafunzo hayo Pamela Mollel amesema kupitia mafunzo hayo wamejengewa uwezo zaidi Katika kuandika habari za mazingira.
“Waandishi wa habari wanaoandika habari za uchunguzi wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo vitisho, kunyimwa taarifa, kunyanyaswa kijinsia, hivyo kupitia mafunzo haya tutajengewa uwezo zaidi wa kuandika habari hizo,” amesema.





