NA DENIS MLOWE, IRINGA
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Salim Abri ‘Asas’, amefika kutoa pole katika msiba wa mzee Fabian Senyela Ngajilo, baba mzazi wa Mbunge wa Iringa Mjini Fadhili Ngajilo na mfanyabiashara maarufu nchini Fred Ngajilo (Fred Vunjabei).
Asas aliwasili katika makazi ya familia eneo la Samora, Iringa, akiambatana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Daud Yassin, ambapo walitia saini katika kitabu cha maombolezo na kuwapa pole ndugu, jamaa na marafiki wa familia ya Ngajilo. Viongozi hao pia walipata nafasi ya kuzungumza na mjane wa marehemu, wakionesha mshikamano na upendo katika kipindi hiki cha majonzi.
HISTORIA FUPI YA MAREHEMU MZEE FABIANI SENYELA NGAJILO (SISI KWA SISI)
KUZALIWA
Marehemu Fabiani Senyela Ngajilo alizaliwa tarehe … (tarehe haijawekwa), katika familia ya watoto 12, akiwa mtoto wa nne kati ya watoto sita wa mama Patricia Ngailo na baba Senyela Ngajilo.
ELIMU
Alianza masomo katika Shule ya Msingi Itagutwa, Iringa, mwaka 1963 na kuhitimu mwaka 1970.
Mwaka 1971 alijiunga na Chuo cha Ufundi Bukoba (Kagera) kusomea Automotive Mechanics.
KAZI.
Baada ya chuo, aliajiriwa SIMBA KAGERA LIMITED kama Afisa Usafirishaji kuanzia mwaka 1971–1974, Bukoba.
BIASHARA
Kuanzia mwaka 1975, marehemu alijiajiri na kuwekeza kwenye sekta mbalimbali, ikiwemo:
1. Biashara ya usafirishaji (malori ya mizigo)
2. Utengenezaji na uuzaji wa nguo
3. Biashara ya miti na uzalishaji wa mbao
4. Uwekezaji wa majengo, ikiwemo nyumba za biashara na kulala wageni
5. Kilimo (mmoja wa wakulima wakubwa Iringa)
6. Uwakala wa kampuni ya Pepsi kwa mikoa ya Iringa na Njombe
NDOA
Alifunga ndoa tarehe 20/09/1978 na Bi Emma Halali Mbilinyi katika Kanisa la Katoliki Consolata–Mshindo, Iringa, na kubarikiwa watoto 8 (wakike 2, wa kiume 5) na wajukuu 11.
IMANI
Alikuwa Mkatoliki hadi Januari 2026 alipohamia Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Mlandege – Iringa.
HAIBA
Marehemu alifahamika kwa:
1. Uchapakazi
2. Upendo kwa watu
3. Malezi bora
4. Uchangamfu
5. Kumcha Mungu
KIFO
Mnamo 28/01/2026, akiwa mkoani Njombe kwenye shughuli zake, alianza kujisikia vibaya na kukimbizwa Hospitali ya Mkoa wa Njombe, ambako ilibainika amepata mshituko wa moyo (Heart Attack).
Alifariki dunia ghafla saa 2:00 asubuhi, siku ya Alhamisi, 29/01/2026, akiwa na umri wa miaka 71 Ameacha mjane, watoto 7 na wajukuu 11.





