Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mwalimu Mhakiki wa Maandishi ya Breli na Michoro ya Mguso kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania Bi. Hadija Salum wakati akitoa maelezo kuhusu matumizi ya michoro ya mguso katika ufundishaji wa watoto wa Elimu ya Awali, Wanafunzi wa Darasa la Kwanza na la Pili, mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), tarehe 29 Januari, 2026.
…………..
Na. John Bukuku – Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali imejipanga kuhakikisha Mpango Mkakati wa Kisayansi wa Kujenga Umahiri wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa watoto wa elimu ya awali na wanafunzi wa Darasa la Kwanza na la Pili unatekelezwa kikamilifu katika ngazi zote nchini.
Akizungumza Januari 29, 2026 jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa mpango huo, Rais Samia alisema Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia itashirikiana kwa karibu na Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI pamoja na wizara za kisekta zinazohusika na malezi na maendeleo ya awali ya mtoto ili kuhakikisha mkakati huo unaleta matokeo halisi kwa watoto.
Alisema Serikali itaimarisha ufuatiliaji na uwajibikaji wa utekelezaji kuanzia ngazi ya shule hadi mikoa, akisisitiza kuwa lengo ni kuona mtoto wa Darasa la Pili anapofikia Darasa la Tatu akiwa na uwezo wa kusoma, kuandika na kuhesabu kulingana na viwango vilivyowekwa.
Rais Samia alibainisha kuwa tathmini za mapema zitafanyika ili kubaini changamoto za wanafunzi na kutoa msaada kwa wakati, huku akitoa wito kwa wazazi, walezi na jamii kushirikiana na Serikali katika kufanikisha malengo ya mpango huo.
Aidha, alisema Serikali itaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa mkakati huo na kuimarisha mifumo na rasilimali, akieleza kuwa ana imani na uongozi wa Wizara ya Elimu unaoongozwa na Profesa Adolf Mkenda katika kufanikisha mpango huo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akionesha Kitabu cha Mpango Mkakati wa Kisayansi wa Kujenga Umahiri wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa watoto wa Elimu ya Awali na Wanafunzi wa Darasa la Kwanza na la Pili mara baada ya uzinduzi katika viwanja vya Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), tarehe 29 Januari, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akionesha Tuzo aliyokabidhiwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Kisayansi wa Kujenga Umahiri wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa watoto wa Elimu ya Awali na Wanafunzi wa Darasa la Kwanza na la Pili katika viwanja vya Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Januari, 2026.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Changanyikeni wakiimba wakati wa hafla ya uzinduzi Mpango Mkakati wa Kisayansi wa Kujenga Umahiri wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa watoto wa Elimu ya Awali na Wanafunzi wa Darasa la Kwanza na la Pili. Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), tarehe 29 Januari, 2026.

Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi Mpango Mkakati wa Kisayansi wa Kujenga Umahiri wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa watoto wa Elimu ya Awali na Wanafunzi wa Darasa la Kwanza na la Pili. Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), tarehe 29 Januari, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kisutu na Shule ya Msingi Changanyikeni mara baada ya kuzindua Mpango Mkakati wa Kisayansi wa Kujenga Umahiri wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa watoto wa Elimu ya Awali na Wanafunzi wa Darasa la Kwanza na la Pili katika viwanja vya Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), tarehe 29 Januari, 2026.
