Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi-CCM, Bara, John Mongella, Januari 31.2026 anatarajia kuanza ziara katika Mikoa ya Shinyanga na Mwanza.

Katika ziara hiyo atazungumza na Mabalozi wa Mashina, viongozi mbalimbali wa CCM na Jumuiya zake, pia atapata fursa ya kutembelea wagonjwa katika Hospitali ya Sekotoure iliyopo Mkoani Mwanza hii ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 49 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi-CCM.