Na Meleka Kulwa – Fullshangwe Blog, Dodoma
Simba SC imeendelea kupata matokeo mabaya katika hatua ya makundi ya mashindano ya CAF Champions League msimu wa 2025/26. Baada ya kufuzu hatua ya makundi, klabu hiyo imecheza mechi tatu bila kupata matokeo mazuri dhidi ya wapinzani wake.
Katika mechi ya kundi D iliyochezwa Januari 24, 2026 nchini Tunisia, Simba SC wamepoteza kwa goli 1-0 dhidi ya Espérance de Tunis ya Tunisia. Goli hilo lilifungwa mapema katika mchezo uliochezwa uwanja wa Radès.
Katika michezo iliyopita, Simba SC ilipoteza kwa goli 1-0 kutoka kwa Petro de Luanda ya Angola katika mchezo wa nyumbani uliofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Kisha wakapoteza kwa 2-1 ugenini dhidi ya Stade Malien ya Mali.
Hadi sasa, Simba SC bado hawajafanikiwa kuvuna alama katika kundi D, na ili wafuzu hatua ya robo fainali wanatakiwa washinde michezo yao yote iliyobaki huku wakiwaombea mabaya wapinzani wao.




