Waziri wa Katiba na Sheria ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Mkoani Ruvuma Dkt. Juma Zuber Homera,akizungumza na wananchi wa kiijiji cha Mlilayoyo kata ya Hanga wakati wa ziara yake ya siku tatu kuzungumza na wananchi wa jimbo hilo.
Meneja wa RUWASA Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma Mhandisi David Mkondya,akitoa taarifa za utekelezaji wa miradi ya maji kwenye vijiji mbalimbali Wilayani humo wakati wa Mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Dkt. Juma Zuber Homera.
Na.Mwandishi Wetu,Namtumbo
WAZIRI wa Katiba na Sheria Dkt Juma Homera amesema,utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo miradi mikubwa ya majisafi na wilayani Namtumbo ni endelevu kwani Serikali kwa kushirikiana na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo imejipanga kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kijamii katika maeneo yao.
Dkt Homera amesema hayo mwishoni,wakati akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Mlilayoyo kata ya Hanga Halmashauri ya Wilaya Namtumbo Mkoani Ruvuma kwenye mkutano wake wa kuwashukuru wananchi waliomchagua kuwa Mbunge wa Jimbo hilo kwenye uchaguzi Mkuu mwaka jana.
Dkt. Homera ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Namtumbo alisema,tayari ofisi yake imeanza kutatua kero kubwa ya maji kwa kununua mabomba 320 yenye thamani ya zaidi ya Sh.milioni 30 kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maji katika vijiji mbalimbali vya Wilaya ya Namtumbo.
Aidha alisema,katika msimu wa kilimo 2025/2026 amegawa mbegu bora za ufuta tani 5,000 zilizotolewa bure kwa wakulima ili walime kwa tija na kuongeza kipato kwa wakulima ikiwa ni mkakati wa kuwakwamua wananchi wa Jimbo hilo na umaskini na kuiwezesha Halmashauri kuingiza mapato yake kupitia zao hilo.
Akizungumzia kuhusu Barabara ya Lumecha-Londo hadi Kilosa kwa Mpepo mkoa jirani wa Morogoro Dkt Homera alisema,tayari mkandarasi amepatikana na punde itaanza kujengwa kwa kilometa 100 kwa kiwango cha lami.
Alisema,Barabara hiyo ni muhimu kwa uchumi wa Mkoa wa Ruvuma hususani wilaya ya Namtumbo kwani itarahisisha sana shughuli za usafiri na usafirishaji wa bidhaa kutoka Mikoa ya Morogoro, Dar es slaam kuja Ruvuma kirahisi zaidi ikilinganisha na Barabara kuu ya Songea-Njombe kupitia Iringa.
Kwa upande wake Meneja wa Ruwasa Wilaya ya Namtumbo David Mkondya alisema,Serikali kupitia Wizara ya maji inaendelea kujenga miradi ya maji 2 yenye thamani ya zaidi ya Sh.bilioni 3.
Mkondya ametaja miradi hiyo ni mradi wa maji Mchomoro utakaohudumia Kijiji cha Mchomoro na Songambele ambapo wakazi 9,000 watanufaika na mradi wa maji Msisima-Mnalawi utakaohudumia vijiji viwili vyenye wakazi zaidi ya 4,000.
Kwa mujibu wa Mkondya,katika kata ya Hanga Kijiji cha Mlilayoyo na Mageuzi Serikali kupitia Ruwasa imekamilisha usanifu wa mradi mkubwa wa maji unaotumia chanzo cha Lipita na mradi huo upo katika bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026.
Kwa mujibu wa Mkondya,katika kata ya Hanga Ruwasa imekamilisha kufanya usanifu wa mradi mkubwa wa maji unaotumia chanzo cha maji cha Lipita utakaohudumia vijiji viwili vya Mlilayoyo na Mageuzi na utaanza kutekelezwa kupitia bajeti yam waka wa fedha 2025/2026.
Mkondya alisema,Ruwasa kwa kushirikiana na ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Namtumbo imepanga kuchimba kisima kirefu kama hatua ya haraka ili kupunguza changamoto ya maji katika Kijiji cha Mlilayoyo.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi Diwani wa kata ya Hanga Reginbert Henjewele,ameiomba Serikali kupitia wakala wa maji na usafi wa mazngira vijijini(Ruwasa),kumaliza changamoto ya majisafi na salama ili kutoa nafasi kwa wananchi waweze kushiriki katika shughuli za maendeleo badala ya kutumia muda mwingi kutafuta huduma hiyo.
Henjewele alisema,kero ya maji katika Kijiji cha Mlilayoyo na vijiji vingine ni kubwa hivyo wananchi wanalazimika kutumia maji kutoka kwenye visima vya asili na kutumia muda mwingi kwenda kutafuta huduma hiyo.
Aidha Henjewele,ameishukuru Serikali na ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Namtumbo kuwajengea kivuko cha kudumu katika Mto Libango unaotenganisha Kijiji hicho na kata nyingine.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Kijiji hicho Henjewele alisema,kivuko hicho kimemaliza mateso ya muda mrefu kuvuka kwenye maji pindi hasa kipindi cha masika pindi wanapotaka kwenda kwenye shughuli za kilimo na vijiji jirani.
Ameipongeza Serikali ya awamu ya sita,kutoa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo mradi wa zahanati na shule ya sekondari huku wananchi kwa kushirikiana na Serikali wameanza kujenga mabweni ya wanafunzi.
“Hata hivyo tunaiomba Serikali itujengee soko ili tuweze kuuza mazao yetu kwa bei nzuri badala ya kuuza kwa walanguzi shambani wanakuja na kununua mazao tunayozalisha kwa bei ndogo isiyolingana na gharama za uzalishaji”alisema Henjewele.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Namtumbo Fransis Mgoloka, amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kupeleka fedha nyingi Wilayani humo ili kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo iliyowezesha wananchi kupata huduma bora za kijamii.
Mgoloka,amempongeza Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Dkt Juma Homera,kwa kuanza kutekeleza ahadi alizotoa kwa wananchi wa jimbo hilo wakati wa kampeni za Uchaguzu Mkuu wa mwaka ikiwemo kupata kituo cha kuuza mbolea




