Dar es Salaam — Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Taifa, Ndugu Othman Masoud Othman, ameongoza kikao cha Kamati Kuu cha chama hicho kinachoendelea muda huu katika Ukumbi wa Hakainde Hichilema, Makao Makuu ya Chama, Magomeni jijini Dar es Salaam.
Kikao hicho muhimu kimewakutanisha viongozi wakuu wa chama kutoka ngazi mbalimbali kwa lengo la kujadili masuala ya kimkakati yanayohusu mwelekeo wa kisiasa wa ACT Wazalendo, uimarishaji wa chama pamoja na agenda za kitaifa.
Miongoni mwa walioshiriki kikao hicho ni aliyekuwa mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia ACT Wazalendo, Ndugu Luhaga Mpina, ambaye amekuwa sehemu ya mjadala unaoendelea ndani ya Kamati Kuu.
Kikao hicho kinatarajiwa kutoa mwelekeo mpya kuhusu masuala ya kisiasa, demokrasia, maslahi ya wananchi na mustakabali wa taifa kwa ujumla.

