Jengo la gorofa tisa linalomilikiwa na Shirika la Hifadhi ya Taifa ya Jamii (NSSF), lililopo eneo la Posta jijini Dar es Salaam, limenusurika kuungua baada ya moto mkubwa kuibuka.
Jengo hilo linalojulikana kwa jina la Hifadhi House, lilikumbwa na tukio hilo la moto leo Januari 16, 2026 majira ya saa sita mchana katika mazingira ambayo bado chanzo Cha moto huo haujafamika.
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama, linaendelea na jitihada za kuzima moto huo pamoja na kuwaokoa watu waliokuwepo ndani ya jengo hilo wakati wa tukio.
Hadi sasa chanzo cha moto huo bado hakijafahamika. Full Shangwe Blog inaendelea kufuatilia tukio hilo kwa karibu, ikiwemo jitihada za kumtafuta Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Ilala pamoja na Uongozi wa NSSF ili kupata taarifa zaidi.





