Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya wanaume ya Mali imefanikiwa kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Zambia katika mchezo wa Michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025, uliochezwa leo Desemba 22, 2025 nchini Morocco.
Mali walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 61 kupitia mshambuliaji Lassine Sinayoko.
Bao la kusawazisha kwa Zambia lilifungwa na Patson Daka katika dakika ya 90+2 ya mchezo huo.
Kufuatia matokeo hayo, Morocco wameendelea kubaki kileleni mwa Kundi A wakiwa na pointi 3, huku Mali na Zambia kila mmoja akiwa na pointi 1. Comoros wanashika nafasi ya mwisho kwenye kundi hilo.
Mchezo WA pili Morocco wataminyana na Mali na Comoros watacheza na Zambia.




