……….
Na Happy Lazaro, Arusha .
JUMLA ya madiwani 34 wa Jiji la Arusha leo wamekula kiapo rasmi kwa ajili ya kuwatumikia wananchi katika kata zao ambapo madiwani 25 walichaguliwa na madiwani nane ni wa viti maalumu.
Akizungumza kwenye halfa hiyo ya uapisho Katibu Tawala Wilaya ya Arusha Mjini, Jacob Rombo amewataka madiwani hao kuhakikisha wanaziba mianya ya rushwa katika maeneo yao hususani katika miradi mbalimbali ya maendeleo.
Aidha Rombo amesema kuwa , ni wajibu wao kwenda kutekeleza ahadi zote walizoahidi kwa wananchi katika kata zao kwani wana matarajio makubwa sana na viongozi hao .
Nawaomba sana mhakikishe mnatanguliza swala la utawala bora kwa wananchi wenu kwani ni muhimu katika kuwaletea maendeleo wananchi ikiwemo kuepuka suala zima la rushwa na kuagiza kuacha kuingilia kati majukumu ya watumishi wanaotekeleza ikiwemo suala la mipango miji.”amesema Rombo.
“Msiingiliane majukumu wakati wa utendaji kazi, Bali mfuate sheria na taratibu za halmashauri, simamieni viapo vyenu”amesema .
Kwa upande wao baadhi ya madiwani akiwemo Diwani Muhsin Ramadan wa kata ya Sokon 1 amesema kuwa atahakikisha anasimamia kikamilifu miradi ya wananchi ikiwemo kufanya kazi kwa weledi mkubwa na uaminifu kama ambavyo wananchi wamemwamini na kumpa nafasi ya kuwaongoza .
Diwani wa kata ya Muriet Kredo Kifukwe amesema kuwa , nafasi aliyopewa na wananchi hao ni kibwa sana na kamwe hatawaangusha bali atahakikisha miradi ya maendeleo inafanyika kwa umakini na weledi mkubwa .
“Ninachowaomba wananchi ni kuhakikisha wananipa wananipa ushirikiano wa kutosha katika kutekeleza majukumu yangu ili kwa pamoja tushirikiane kuitengeneza Muriet mpya ambayo itakuwa ya mfano.”amesema Kifukwe .
Michelle Mrema amesema kuwa atasimamia vema majukumu yao ikiwemo kufanya kazi kwa ufanisi katika kuleta maendeleo kwa wananchi wa kata 25 za Jiji la Arusha.





