WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST) Prof.Adolf Mkenda,akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 26,2025 jijini Dodoma kuhusu ya maadhimisho ya miaka 50 ya kuanzishwa kwa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW),yanayotarajiwa kufanyika jijini Dar es salaam.

Na Alex Sonna, Dodoma
NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati , Mhe. Dkt. Doto Biteko ,anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) yatakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Agosti 25 hadi 27, 2025.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amesema maadhimisho hayo yatatanguliwa na wiki tatu za shughuli mbalimbali za elimu na uhamasishaji wa jamii kuhusu elimu ya watu wazima na nje ya mfumo rasmi.
“Maadhimisho haya ni ya kihistoria. Yanalenga kuonesha mafanikio ya TEWW katika miaka 50 ya utoaji wa elimu jumuishi, kujadili changamoto zilizopo na kuweka mwelekeo wa baadaye,” alisema Prof. Mkenda.
Kwa mujibu wa Waziri huyo, kauli mbiu ya mwaka huu ni “Elimu bila ukomo kwa maendeleo endelevu”, ikilenga kuhamasisha jamii kujifunza bila kikomo, kujikita kwenye maarifa ya ujasiriamali, ufundi na uboreshaji wa maisha kwa watu wazima na vijana waliopo nje ya mfumo rasmi.
Prof. Mkenda alibainisha kuwa katika siku ya kwanza ya kongamano,Naibu Waziri Mkuu Dkt.Biteko atazindua rasmi maadhimisho hayo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), huku kilele chake kikitarajiwa kufungwa mnamo Agosti 27, 2025.
Aidha, Prof. Mkenda alisema kutakuwa na mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo Maafisa Magereza na Wakufunzi wa TEWW yatakayofanyika Julai 28–30 jijini Dodoma, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha elimu ya kisomo kwa wahitaji walioko magerezani.
Katika kuelekea kilele hicho, kutafanyika maonesho ya elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi yatakayowakutanisha wadau zaidi ya 1,000 kutoka ndani na nje ya nchi. Maonesho hayo yatafanyika JNICC kuanzia Agosti 24 hadi 27, yakihusisha taasisi za umma, binafsi, wajasiriamali na vijana waliopitia mfumo huo.
Baadhi ya huduma zitakazotolewa kwenye maonesho hayo ni pamoja na ushauri, udahili wa kozi mbalimbali, uoneshaji wa bunifu, bidhaa na ujuzi wa wanafunzi wa elimu isiyo rasmi.
“Tunawahamasisha Watanzania wote, hususan vijana, wanawake na watu wazima waliokosa fursa ya elimu ya msingi na sekondari, kufika kujifunza, kujiunga na kushiriki kwenye maonesho haya ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa,” alisisitiza Prof. Mkenda.
Waziri huyo pia alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wadau wote wa ndani na nje ya nchi kwa ushirikiano wao katika mafanikio ya miaka 50 ya TEWW na kwa kukubali kushiriki kwenye maadhimisho hayo.