MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Mboni Mhita,akizungumza na Waandishi wa Habari leo Julai 14,2025 jijini Dodoma kuhusu Mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita kwa kipindi cha Novemba 2020 hadi April 2025.

SEHEMU ya Waandishi wa habari wakifatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Mboni Mhita,(hayupo pichani) wakati akizungumza kuhusu Mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita kwa kipindi cha Novemba 2020 hadi April 2025.

Na Alex Sonna-DODOMA
MKOA wa Shinyanga umeibuka kuwa nguzo ya ukuaji wa uchumi wa Taifa kupitia usimamizi madhubuti wa rasilimali zake, ukusanyaji mapato na utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati, chini ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita ameeleza hayo leo July 14,2025 jijini Dodoma wakati akieleza mafanikio ya Mkoa huo kwa kipindi cha miaka minne ambapo amesema Mkoa huo umekusanya zaidi ya shilingi bilioni 540.17 kutoka sekta ya madini pekee, na bilioni 202.54 kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ikiwa ni asilimia 102 ya lengo.
“Ukusanyaji wa mapato umekuwa chachu ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati, ikiwemo uboreshaji wa hospitali, miundombinu, elimu, maji na umeme kwa wananchi wetu,” amesema Mhita.
Amesema Mkoa umefanikiwa pia kutekeleza miradi ya maendeleo ya thamani ya bilioni 65.5 kwa kutumia mapato ya ndani ya halmashauri, hatua inayodhihirisha ufanisi wa usimamizi wa fedha za umma kwa maendeleo ya watu.
Kwa upande wa sekta ya madini,amesena uzalishaji umeongezeka mara tano kutoka tani 7.9 mwaka 2020 hadi tani 42.5 mwaka 2025, na mapato ya halmashauri kutokana na madini yakipanda kutoka milioni 745.4 hadi bilioni 3.3. Vituo vya ununuzi wa madini vimeongezeka kutoka sita hadi 12, na leseni kwa wachimbaji wadogo kutoka 332 hadi 1,766.
“Tunathamini mchango wa wachimbaji wadogo na wawekezaji wa madini kwa ustawi wa uchumi wetu. Hii ndiyo maana Mkoa wetu umewekeza katika miundombinu rafiki ya sekta hiyo,” amesisitiza Mhita.
Kwa upande wa nishati, amesema Serikali kupitia TANESCO imetumia shilingi bilioni 492 kuunganisha vijiji vyote 506 vya mkoa huo kwenye umeme, na kusambaza mitungi 6,500 ya gesi ili kuendeleza matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Mkuu wa Mkoa huyo amebainisha kuwa Shinyanga sasa ni kitovu kipya cha uwekezaji, kufuatia hatua ya Serikali kupima zaidi ya viwanja 10,000 na kuandaa maeneo ya uwekezaji katika maeneo ya Chapulwa, Zongomela, Negezi na Ibadakuli.
Katika hatua nyingine,ameeleza kuwa Mkoa unaendelea na utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati kama vile Mradi wa Umeme Jua (MW 150) Ngunga – bilioni 323,Uboreshaji wa Kiwanja cha Ndege Ibadakuli – bilioni 52.87,Barabara ya Kahama-Bulyanhulu-Kakola (km 73) – bilioni 100.6 na Mradi wa TACTIC wa viwanda, masoko, barabara na stendi Kahama na Shinyanga – jumla ya bilioni 72.6
“Kwa sasa, Mkoa unaendelea kushiriki kikamilifu katika maonesho ya kibiashara ikiwemo Sabasaba ya Dar es Salaam, na kuitangaza Shinyanga kama fursa ya biashara, uwekezaji, uchimbaji, viwanda na kilimo chenye tija, ” ameeleza na kuongeza;
“Shinyanga sasa si tu ni mkoa wa historia ya madini, bali ni mfano wa mapinduzi ya kiuchumi kupitia uongozi wenye dira na uthubutu,” amesema Mhita.