Mwamvua Mwinyi, Kibaha
Julai 4, 2025
Jumla ya wanawake 33 wametia nia kuwania nafasi za Ubunge, kupitia Viti Maalum na Makundi Maalum ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ,Mkoa wa Pwani.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwakek Julai 3,2025 ,mjini Kibaha Katibu wa Siasa ,Uenezi -Mafunzo wa CCM ,Mkoa wa Pwani, David Mramba alisema kuwa, majina ya watia nia yanapelekwa Makao Makuu ya chama jijini Dodoma kwa hatua zaidi.
Mramba alieleza ,majina hayo yatapitiwa na kurejeshwa mkoani ambapo mchakato wa vikao mbalimbali vya chama vinaanza Julai 4 mwaka huu.
Alifafanua kuwa ,mchakato huo umekwenda kwa utulivu na uwazi na hatua inayofuata ni kusubiri majina yatakayopitishwa ili taratibu nyingine ziendelee.
Kwa mujibu wa Mramba wanachama waliotia nia kugombea Ubunge kupitia Viti Maalum ,ni Sifa Mwaruka ,Rehema Issa ,Zainab Vullu ,Joan Tandau ,Khadija Ismail ,Julieth Shio ,Janeth Mogeni, Mariam Ibrahim, Fatuma Msumi ,Nancy Mutalemwa ,Mwashabani Puga, Irene Makongoro, Jamila Mkumbwa ,Hawa Chakoma na Rehema Msemo.
Kwa upande wa Makundi Maalum waliotia nia ,ni Dk .Hawa Mpate, Zamda Komba, Bahati Zongo ,Tungi Mwanjala, Hawa Mcheka, Asha Baraka ,Suzan Mdonya ,Nuru Abdala ,Esta Mangana, Betha Mungure na Judith Mjale.
Aidha Mramba alibainisha ,idadi ya madiwani waliotia nia kugombea Viti Maalum katika halmashauri mbalimbali za Mkoa wa Pwani , kwa upande wa Kibaha Mjini 34, Kibaha Vijijini 39, Bagamoyo 37, Mkuranga 51, Kisarawe 20,Kibiti 20, Rufiji 22 na Mafia 12.
Kwa upande wa Kata ,idadi ya watia nia kwa mujibu wa jinsia ni Kibaha Mjini 94, wanaume 77 wanawake 17, Kibaha Vijijini 100 ,wanaume 73 wanawake 27, Bagamoyo 173 wanaume 138 wanawake 35 Mkuranga 181 wanaume 139 wanawake 42, Kisarawe 94 wanaume 70 wanawake 24, Kibiti 72 wanaume 65 wanawake 7, Rufiji 190 wanaume 187 wanawake 13 na Mafia 43 wanaume 41 wanawake 2.
Mramba aliwataka watia nia wote, kufuata taratibu za chama na kutoanza kampeni kabla ya muda rasmi huku akisisitiza kuwa mwanachama yeyote atakayebainika kukiuka maadili ya chama atachukuliwa hatua kwa mujibu wa kanuni.