Sajenti Emmanuel Kisiri ambae ni polisi kata wa kata ya Ikoma Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara ameendelea kuihimiza jamii kulinda maadili ya watoto
Akiendelea na kampeni yake ya Nyumba kwa Nyumba katika kijiji cha Robanda kitongoji cha Momorogoro kata ya Ikoma Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara Sajenti Emmanuel aliwakumbusha wazazi na walezi mambo yafutayo:
Kumchapa mtoto viboko vichache ni kumfundisha mtoto tofauti ya jema na baya huku wakitumia lugha ya upendo kwa kumweleza mtoto kwa upole juu ya makosa yake
Wazazi kutenga mda wa kuzungumza na watoto wao kila siku na pia kuwapa nafasi ya kuongea bila kumkataza mtoto huku ukimuonyesha mtoto kwamba hisia zake ni muhimu
Na mwisho aliwakumbusha wazazi kua michezo mbalimbali kwa mtoto si kupoteza muda ni njia ya mtoto kujifunza, kujenga ubunifu, na kuendeleza uhusiano mzuri na wenzake ivyo basi aliwasihii wazazi kuwaruhusu watoto kucheze ila wakiwa kwenye uangalizi wao ili watoto waufurahie utoto wao.