Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Selemani Jafo Serikali itaendelea kulinda na kukuza viwanda vya ndani kwa kuweka mazingira wezeshi na rafiki kwa biashara na uwekezaji ili kuongeza ajira, Pato la Taifa na kukuza uchumi Jumuishi kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Aidha, Waziri Jafo ametoa wito kwa Wazalishaji Kundelea kutumia malighafi za ndani Katika kuzalisha bidhaa mbalimbali kama TCC anavyozalisha bidhaa zake kwa kutumia malighafi kutoka kwa wakulima wa Tanzania
Ameyama hayo Julai 03, 2025 alipotembelea Kampuni ya Sigara Tanzania ambayo ni kampuni tanzu ya JTI (Japan Tobacco International) jijini Dar es Salaam akiwa ameambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Suleiman Serera na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwanda Bw. Juma Mwambapa kwa lengo la kujifunza shughuli za uzalishaji na kusikiliza changamoto zao.
Waziri Jafo pia ameipongeza Kambuni hiyo kwa uzalishaji mzuri unaojumuisha mnyororo wa thamani wa Tumbaku kuanzia kwa Mkulima hadi Kiwandani kwa kutumia malighafi zilizopo nchini hatua inayosaidia kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira nchini.
Naye Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Tanzania Sigara Tanzania (TCC), Bi. Patricia Mhondo, amebainisha kuwa shughuli za TCC zinagusa maisha ya watu nchini kupitia mnyororo wa thamani unaowahusisha wakulima, wazalishaji, wauzaji na wasambazaji.
“Kwa maana hiyo, kampuni yetu inaleta ajira kwa watu wengi zaidi ya wale waliopo ndani ya TCC moja kwa moja. Hii inachangia kukuza uchumi wa nchi na kuongeza mapato ya Serikali kupitia ulipaji wa kodi,”
Aidha, alitumia fursa hiyo kutoa shukrani kwa Waziri wa Viwanda na Biashara kwa kutembelea kiwanda hicho na kufanya mazungumzo nao kuhusu mafanikio ya kampuni na changamoto wanazokumbana nazo.