Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akifanya mazungumzo na Mjumbe wa Ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani Balozi Susanne Wusan-Rainer kando ya Mkutano wa Nne wa Kimataifa kuhusu Ufadhili wa Maendeleo (FfD4) unaofanyika Jijini Sevilla nchini Hispania. Tarehe 01 Julai 2025.