Mratibu wa Mashindano Yustino Mdesa
DENIS MLOWE,IRINGA
MASHINDANO ya Ilolo Mpya Sabasaba Super Cup yameingia rasmi mkataba wa miaka 8 kwa kuweza kudhaminiwa na mdau wa maendeleo ambaye pia mkuu wa wilaya mstaafu wa Monduli Festo Kiswaga
Awali mdhamini Festo Kiswaga ambaye ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Ccm kutokea Iringa Vijijini alikuwa akitoa fedha tangu mwaka 2022 kwa kutoa zawadi kwa washindi hali ambayo kutokana na maombi ya waratibu wa mashindano hayo ameingia rasmi kudhamini kwa kutoa milioni 10 kwa ajili ya kufanikisha mashindano hayo
Akizungumza mbele ya waandishi wa Habari Mratibu wa Mashindano hayo Yustino Mdesa alisema kuwa udhamini huo ulianza tangu 2022 kwa Mjumbe wa Kamati Kuu Ccm kutokea Iringa Vijijini kwa kutoa zawadi kwa washindi na kusema kuwa mkataba huo utakuwa unaongezeka kwa kiwango cha fedha kila mwaka hadi 2030.
Alisema kuwa kila mwaka zawadi za mashindano hayo zitapanda ambapo kwa mwaka huu bingwa atajinyakulia milioni 3 kitu ambacho hakijawahi tokea kwa jimbo la Ismani kuwa na mashindano yenye zawadi kubwa kiasi hicho kinachotolewa na mdau wa maendeleo na Dc mstaafu Festo Kiswaga.
Aliongeza zaidi kuwa lengo la mashindano hayo ambayo yameshafanyika kwa miaka 16 ni kuvumbua vipaji ambapo katika miaka yote tangu kuanza kwa mashindano kuna wachezaji mbalimbali wameshatoka kimpira mmoja wapo Clement Mzize alikwishapita katika mashindano hayo
Alisema katika mashindano ya mwaka huu wameongeza zawadi tofauti na msimu uliopita ambapo kwa sasa bingwa wa mashindano hayo ataibuka na kitita cha milioni 3 , mshindi wa pili ataibuka na milioni 1.5 atakayeshika nafasi ya tatu ataibuka na laki 5 wakati nafasi ya nne laki 2.
Aliongeza kuwa katika udhamini wa Festo Kiswaga msimu huu kutakuwa na zawadi kwa timu yenye Nidhamu ambapo itaondoka na laki 2 Mfungaji bora laki 1 kipa Bora Tsh laki 1.
Mdesa alimshukuru mdhamini mkuu wa mashindano hayo Festo Kiswaga kwani kitendo alichofanya ni cha uzalendo kuweza kuwekaza fedha kikubwa katika mashindano hayo ambayo yamekuwa makubwa na ushindani kwa sababu yake hivyo katika kufanikisha zaidi mashindano hayo mdhamini aliweza kutoa jezi kwa zote 16 zilizoshiriki mashindano hayo zenye thamani ya milioni 3
Katika hatua nyingine timu 8 zimefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ambapo Juni 28 kutakuwa na mchezo wa kwanza kati ya
Chicago fc vs Mboliboli fc mchezo utakaopigwa katika uwanja wa Ilolo mpya.
Timu nyingine zilizofuzu hatua ya robo fainali ni timu za Leopard fc vs Nyota fc watakaokutana Juni 29, Makuka fc vs Kinyika fc hawa wataumana Julai mosi na mtanange wa mwisho utakuwa kati ya Mbugani fc vs Mlowa stars