Waziri wa Uchukuzi prof Makame Mbarawa awasilisha ripoti maalumu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM kwa miaka mitano jimbo la Mkoani Pemba
Akiongea na Viongozi pamoja na wanachama mbalimbali wa chama hicho Prof Mbarawa amebainisha namna alivyofanya jitihada za ziada kwa kutafuta pesa kutoka kwa wadau wake ili kukamilisha miradi mbalimbali ya jimbo, ambapo zaidi ya Tsh Milioni 800 zimetumika katika kipindi cha miaka mitano ya Ubunge wake.




