Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Kaskazini, Mhandisi Lorivii Long’idu,akizungumza wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wasambazaji na wauzaji wa gesi ya kupikia (LPG) Jiji la Arusha.

Wasambazaji na wauzaji wa gesi ya kupikia (LPG) Jiji la Arusha wakifuatilia mada mbalimbali katika semina hiyo
Happy Lazaro,Arusha .
Arusha .Wauzaji wa mitungi ya gesi ya rejareja wametakiwa kufanya biashara hiyo kwa kufuata kanuni na sheria zilizopo kwa kuwa na mizani maalumu.kwa ajili ya kupimia ujazo uliopo kwenye mitungi ya gesi kabla ya kumwuzia mteja .
Hayo yamesemwa na Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Kaskazini, Mhandisi Lorivii Long’idu,akizungumza wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wasambazaji na wauzaji wa gesi ya kupikia (LPG) Jiji la Arusha.
‘Tunaomba sana mhakikishe mnakuwa na mizani na mizani hiyo iwe imehakikiwa na wakala wa vipimo hapa nchini kwani malalamiko yaliyopo ni makubwa sana kwa wananchi ya kuuziwa mitungi isiyokuwa na ujazo sahihi na sio vinginevyo.”amesema Long’idu.
“sisi tutapita kwenye maeneo yenu kwa ajili ya kukagua kama kweli mnatumia hizo mizani na kutumia mizani hii ni ili kutudhibitishia kuwa kiwango cha gesi kilichopo kwenye ule mtungi ndicho mteja anakipata na sio vinginevyo .”amesema .
Aidha amewataka wafanyabiashara wanaowauzia wananchi gesi ya kupikia moja kwa moja majumbani kuhakikisha kwamba wanafuata zile taratibu na mteja halalamiki na kupata kiwango sahihi cha gesi kilichoandikwa kwenye ule mtungi hivyo tumewakumbusha wajibu wao wa kuwa na mizani ya kupimia ile mitungi na kumuuzia mteja mtungi ambao una kiwango sahihi kama inavyoonekana .
“Unapomtuma boda boda wako akichukulie mtungi wa gesi mwambie yule muuzaji akupimie mtungi na uhakikishe kiwango unachotaka kimesoma kwenye mizani na hii itakusaidia ww kupata kiwango cha gesi kilichopo kule ndani .”amesema
“Tunawakumbusha wafanyabishara wote wanaofanya biashara kwa kutozingatia hizi Sheria ya kutokuwa na mizani hilo ni kosa kubwa na tunataka mwanachi anapofika eneo kama hilo na kuuziwa mtungi usio salama au sahii kulingana na kiwango wanachohitaji wawasiliane mara moja na mamlaka husika na watachukua hatua stahiki kwa hao wafanyabishara.”amesema .
Long’idu amesema kuwa ,tunaposema nishati tunamaanisha maswala mazima ya umeme ,gesi ya kupikia majumbani, mafuta ya dizeli na mafuta ya magari ambayo yanatumika kwenye vyombo vya moto haoa nchini.
“Leo hii kanda ya kaskazini tumekutana na wafanyabishara wanaouza gesi ya kupikia majumbani katika mkoa wa Arusha tumewaita kama wadau wetu muhimu sana kwenyw sekta hii ya nishati .”amesema
Ameongeza kuwa ,moja ya mkakati wa seikali ya awamu.ya sita kuhusu matumizi ya nishati safi inatoa mwelekeo au dhima kwamba itakapofika mwaka 2034 asilimia 80 ya watanzania waweze kutumia nishati safi kwa ajili ya matumizi ya majumbani mwao na gesi ya kupikia majumbani au gesi ya mitungi ni moja ya bidhaa tunaiita nishati safi .
“Tunachokifanya sisi kama wadhibiti leo ni kukutana na wadau hapa ambao ni wasambazaji wakubwa na wale wauzaji wadogo kwa lengo la kuwakumbusha wajibu na taratibu za ufanyaji wa hii biashara na pia kusisitiza maswala mazima ya usalama kwani gesi ya kupikia majumbani isipotunzwa vizuri inaweza ikaleta madhara .”amesema .
“Lakini vile vile watambue kuwa wanatakiwa kushiriki katika mpango huu wa serikali kwamba itakapofika mwaka 2034 basi asilimia 80 ya watanzania waweze kutumia nishati safi ambayo ni (LPG) ambayo inatokana na zao la mafuta.”amesema .
Amefafanua kuwa leo wamekutana hapa kwanza kuonyesha umuhimu wao kuwa ni wadau muhimu lakini kuwataka wazingatie taratibu kanuni na Sheria kwani tumekuwa tukiona changamoto mbalimbali ambazo wananchi wamekuwa wakilalamika ikiwemo kuuziwa mitungi isiyokuwa na kiwango ambacho kipo kwenye ule mtungi kwa maana ya uchakachuaji .
“Tumewaeleza taratibu ni nini na hatua ambazo sisi tunazichukua ili kuhakikisha kuwa wanazingatia hizo taratibu moja ya hatu ambazo tutachukua ni kuwapiga faini pale watakapokutana wanamwuzia mteja mtungi ambao una kiwango ambacho sio sahihi lakini pia mitungi ambayo haina sild”amesema
Amesema kuwa wanafanya semina hiyo kwani wanaelewa gesi ya kupigia majumbani (LPG) ni moja ya nishati safi ambazo zinatakiwa wananchi wazitumie na ina manufaa mengi na moja ya manufaa hayo ni ulinzi wa mazingira.
“Tumekuja kuwaelimisha na kuwataka wananchi wajue kuwa bidhaa hii ya gesi ya kupikia majumbani ni bidhaa bora na salama na ina manufaa makubwa sana kwenye mazingira afya na pia kwenye jamii pia .”amesema .
“Tumekutana nao ili kukumbushana na kuona hii biashara wanayofanya ni biashara muhimu na ina manufaa mengi ikiwemo ya kimazingira kiafya na kijamii hivyo wananchi watakapoweza kuelimika na wakiweza kuliona hili mtazamo wa serikali kwamba ifikapo 2034 asilimia 80 ya watanzania watakuwa wamehama kutoka kwenye kutumia nishati ambayo sio safi na kwenda kutumia nishati safi na hilo ndio lengo kuu la kukutana leo na hawa wadau na wana wajibu wa kuhakikisha kuwa wanawekeza vizuri na kuzingatia maswala ya kiusalama wanapofanya biashara hiyo “amesema .
Aidha amewakumbusha wafanyabishara kuwa ni kosa kisheria kuuza mtungi ambao hauna kiwango sahihi hilo ni kosa na tumekuwa tukiendelea kuchukua hatua mbalimbali na tunaendelea kuchukua hatua mbalimbali na.moja ya hatua ni kuwanyanganya leseni au kuwasimamisha wasifanye hiyo biashara.
Kwa upande wake Mhandisi wa Petroli Magreth Mwita pia amewataka washiriki utaratibu sahihi wa kupata leseni kwa ajili ya kusambaza au kuuza LPG, na kuzingatia matakwa ya kisheria na ya kiufundi ili kuhakikisha usalama wa watumiaji na uendelevu wa biashara.
.
Kwa upande wao baadhi ya washiriki katika semina hiyo ,Muuzaji na msambazaji wa gas ,Nganashe Laizer wamesema kuwa,semina hiyo ni.muhimi.sana kwao kwani imewawezesha kukumbushana wajibu wao katika utendaji.kazi.ikiwemo kufuata kanuni na taratibu za mamlaka hiyo na hivyo kuahidi kwenda kufanya mabadiliko makubwa kwa wananchi wao kwa kufuata Sheria na kanuni zilizopo.