Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC) Bw.David Kafulila,akitoa mafunzo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC) yaliyofanyika leo Juni 10,2025 bungeni jijini Dodoma.
Na Alex Sonna, Dodoma
Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC) kimetoa mafunzo maalum kuhusu ubia wa sekta hizo mbili (PPP) kwa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC).
Mafunzo hayo yamelenga kuwawezesha wajumbe wa kamati kuelewa kwa kina dhana ya PPP, sheria na mwongozo wake, pamoja na namna bora ya kusimamia, kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa miradi ya ubia kati ya Serikali na sekta binafsi.
Akizungumza katika mafunzo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa PPPC, David Kafulila, amewaeleza wajumbe wa Kamati hiyo kuhusu fursa zilizopo katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati kupitia ushirikiano wa PPP, ikiwa ni pamoja na kuongeza ufanisi wa utoaji huduma, kuchochea ukuaji wa uchumi, na kupunguza mzigo wa kifedha kwa Serikali kupitia uwekezaji kutoka sekta binafsi.
Hata hivyo, amesema ni muhimu kuwa na sheria moja ambayo itakuwa inatumiwa na mamlaka zote katika masuala ya PPP badala ya kila mamlaka kutumia sheria zao kuingia miradi ya ubia.
“Hatua hii itasaidia mamlaka zote kutekeleza miradi ya ubia kwa kutumia sheria moja ya ubia, kwasababu sheria ile ambayo inaunda taasisi zao haijaspecialize kwenye masuala haya ya ubia kwa hiyo kunakuwa na nafasi kubwa ya kutokupata mikataba mizuri ukilinganisha na kama wangetumia sheria mama ya masuala ya ubia,”amesema.
Naye, Makamu Mwenyekiti wa PIC, Mary Masanja, ameomba serikali iendelee kutilia msisitizo katika PPP na kwamba kamati inataka kiongezewe nguvu kituo kiwe mamlaka ili kujitosheleza katika uendeshaji wa shughuli za ubia.
“Kwa sababu ukiangalia kazi zake inasimamia za matrilioni ya fedha lakini hawa watu hawana meno ya kutosha. Na sisi kama kamati tumeliona hili tutendelea kuwasemea na kuishauri serikali wawe mamlaka kamili kwa sababu tunakoenda tunaiona nuru.”
“Lakini ukiangalia kwenye masuala ya ubia kwetu sisi kama Tanzania bado tuko nyuma sana tunahitaji msukumo mkubwa , leo hii tukisema kila kitu serikali ifanye tunachelewa sana dunia sasa hivi haiko huko. Sasa hivi ni PPP, ndoa inafungwa mwekezaji anakuja sisi tunabaki kufuatilia na kuangalia utekelezaji,”alisema.
Kwa upande wake, Mjumbe wa Kamati hiyo, Nicholaus Ngassa, amesema moja ya changamoto zinazokikabili kituo hicho ni taasisi nyingi za serikali kuingia kwenye mikataba wawekezaji kwa utaratibu wa PPP kupitia sheria za taasisi zao licha ya kuwapo kwa sheria ya PPP ambayo imeipa mamlaka PPPC katika kuingia ubia wa sekta binafsi na sekta ya umma.
“Kwa hiyo tutashauri serikali ili haya mambo yaweze kupata uratibu mzuri, kituo kiwezeshwe mikataba yote ya ubia kati ya sekta binafsi na sekta ya umma, isimamiwe na hiki kituo kwa kuwa itaweka utaratibu mzuri lakini pia na ufuatiliaji na tija itatokea kwa sababu itapunguza changamoto mbalimbali ambazo zinajitokeza kwenye mikataba inayoingiwa na wabia,”amesema.
Amesema kwa kuwa Bunge lina wajibu badilisha sheria ya kutunga sheria, watashauri Ofisi ya Spika kuangalia suala hilo lilitwe bungeni ili masuala yote ya ubia yapitie Kituo hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC) Bw.David Kafulila,akitoa mafunzo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC) yaliyofanyika leo Juni 10,2025 bungeni jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC) Bw.David Kafulila,akitoa mafunzo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC) yaliyofanyika leo Juni 10,2025 bungeni jijini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC) Mhe.Mary Masanja,akizungumza wakati wa mafunzo yaliyotolewa na Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC) yaliyofanyika leo Juni 10,2025 bungeni jijini Dodoma.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC) wakifatilia mafunzo yaliyotolewa na Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC) yaliyofanyika leo Juni 10,2025 bungeni jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC) Bw.David Kafulila,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mafunzo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC) yaliyofanyika leo Juni 10,2025 bungeni jijini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC) Mhe.Mary Masanja,akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya mafunzo yaliyotolewa na Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC) yaliyofanyika leo Juni 10,2025 bungeni jijini Dodoma.