Meneja site Joshua Yohana  akionyesha bidhaa mbalilmbali.zinazopatikana kwenye kampuni hiyo jijini Arusha.
Meneja site wa kampuni hiyo Joshua Yohana akitoa maelezo kwa mgeni aliyewatembelea banda lao  kujua huduma wanazotoa
………….
Happy Lazaro, Arusha
Kampuni ya Gadgetronix(GX)  iliyopo jijini Arusha  inayojishughulisha na utoaji wa huduma mbalimbali ikiwemo ya umeme jua imekuja na suluhisho  kwa wadau wa utalii wenye  Lodges na Camps kwa kuja na  Semitrela  ya matairi mawili yenye mfumo wa  umeme jua  unaotembea “Portable solar power system “.
Aidha programu  hiyo wamekuja nayo kwenye maonesho ya utalii ya KARIBU-KILIFAIR  mwaka huu ambapo kwa mwaka jana walikuja na system yenye tairi moja hivyo kwa mwaka huu wamejipanua zaidi kulingana na mahitaji ya wateja wao.
Aidha kifaa hicho ambacho ni “Portable solar power system “kimetengenezwa   kwa kulenga  Camps  zote zinazohamishika (moving camps).
Aidha system hiyo ni kwa ajili ya  Camps ambazo zinahamahama na unapoweka mahema unaweka miundombinu ya maji umeme sasa unapotaka kuhama inakulazimu kuanza kuondoa hivyo vitu hali ambayo ni changamoto kubwa sana  kutokana na kutumia gharama kubwa ya kuanza kuhamisha vitu mbalimbali ila uwepo wa system hiyo  unarahisha  kuhama nayo.kama.ilivyo kwani ni semitrela lenye matairi mawili  na bila kuathiri chochote. 
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho hayo ,Meneja site,Joshua Yohana amesema kuwa ,kampuni hiyo  inajihusisha na utatuzi wa changamoto mbalimbali kwa ajili ya watanzania ambayo inahusisha maswala ya sola.
“kwa mwaka jana tulikuja na kifaa hicho kikiwa na tairi moja na tulifanikiwa kuuzia wateja na mrejesho ulikuwa mzuri sana.”amesema .
Amesema kuwa, kwa  upande wa sola wamekuwa wakifanya na wateja  hasa upande wa lodges na Camps ambazo zipo kwenye hifadhi mbalimbali Serengeti,Tarangire,Ngorongoro, ambapo wamekuwa wakiwafungia sola kwa ajili ya kupata  umeme  jua kwenye maeneo yao .
Amesema kuwa, sola hizo zinakuwa na uwezo mbalimbali na hivyo wanafungia wateja wao kulingana na uhitaji wa mteja mwenyewe.
Ameongeza kuwa, endapo mteja atahitaji power system ya sola kwa ajili ya kuhudumia lodge nzima huwa wanawafungia kwa ubora wa hali ya juu na kuweza kuhudumia wageni wao .
“Zaidi sisi tunawafikia mtu mmoja mmoja kuanzia mtu binafsi, ofisi, viwanda,na  biashara na kwa wananchi wa kawaida pia wanakuwa suluhisho za changamoto mbalimbali kulingana na uhitaji wa mteja mwenyewe .”amesema .
“Katika maeneo ya vijijini tumeweza kufunga sola nyingi sana na kuwezesha wananchi kutotumia jenereta badala yake wanatumia sola kwa ajili.ya matumizi yao mbalimbali .”amesema Joshua .
Aidha amesema kuwa  kampuni hiyo.imekuwa ikifunga sola,geti za umeme,inteneti ,kufunga kamera za ulinzi, kufunga mifumo ya maji moto wa jua,pump za jua ,na pia wanafunga taa za barabarani za sola na umeme ,wanauza friji za umeme na sola  na wanatoa huduma ya umeme jua unaotembea na pia wana chumba cha baridi .
Amefafanua kuwa ,wanafanya kazi katika maeneo mbalimbali na  mikoa.yote kutokana na huduma nzuri wanayotoa ambapo wana matawi yao  Zanzibar ,Dar es Salaam,na nchini Kenya pia .
Amesema kuwa wamekuwa wakitoa suluhisho la changamoto mbalimbali kwani wanachofanya kwa wateja wao ni kuuza suluhisho la changamoto za wateja wao.
“Tulifikia hatua ya kuja na hiki kifaa ambacho ni trela yenye system zote za umeme wa jua ambacho kitamwezesha kuhama nacho popote pale anapohitaji kwenda bila gharama yoyote na kwa muda muafaka ambapo system  ya mwaka huu ina KW 24 na inaweza kubeba WAT 24,000,
hii inakupa umeme kambini na inatumika.maeneo ambayo hakuna umeme kabisa .
Ameongeza kuwa,  hiyo system inaendeshwa na umeme jua na ikatokea jua hakuna system hiyo inaingiliana na jenereta.