Makamu Mwenyekiti CCM Bara Komred Stephen Wasira ameanza ziara ya kikazi mkoani Ruvuma ambayo inatarajia kukamilika Juni 12 mwaka huu. Katika uwanja wa ndege wa Songea Wasira amepokewa na viongozi mbalimbali wa chama na serikali wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Komred Oddo Mwisho na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed