Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuma salam za rambirambi kwa Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Hakainde Hichilema kufuatia kifo cha Rais mstaafu wa Zambia Marehemu Edga Chagwa Lungu
Taarifa iliyotolewa na mtandao wake wa Instagram imesema
“Nimesikitishwa sana kusikia taarifa za kifo cha Rais wa zamani wa Jamhuri ya Zambia, Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu.
Kwa niaba ya Serikali na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, natuma salamu za rambirambi za dhati kwa Mheshimiwa Hakainde Hichilema, Rais wa Jamhuri ya Zambia, familia ya Rais Lungu, marafiki na wananchi wote wa Zambia.
Roho yake ipumzike kwa amani.”