Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza katika mkutano huo jijini Arusha
Happy Lazaro,Arusha .
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro amesema kuwa Sheria za Nchi haziendi likizo kipindi cha kampeni za uchaguzi bali zinakuwepo na zinapaswa kufuatwa kama inavyotakiwa.
Ndumbaro ameyasema hayo wakati akifungua Mafunzo ya Sita kwa Mawakili wa serikali zaidi ya 600 kutoka Wizara,Taasisi na Mamlaka mbalimbali za umma .
“Mwaka huu ni Mwaka wa uchaguzi,
Aidha Mhe. Ndumbaro amewataka mawakili hao kuwaelimisha wanasiasa juu ya kuzingatia Sheria katika kipindi cha Kampeni Kama ambavyo Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara 13 (1) inavyozungumzia usawa mbele ya sheria.
Dkt.Ndumbaro ameongeza kuwa mwanasiasa ama mtu yeyote atakaye kiuka sheria za nchi katika kipindi cha kampeni atahesabika mhalifu kama wahalifu mwengine, kwani uchaguzi ni zoezi la kikatiba.
Aidha mkutano huo umeenda abamba na uzinduzi wa mifumo ya usajili, chapa ya Wakili mkuu wa serikali na maktaba mtandao itakayochochea masuala ya Tehama na Ukuaji wa uchumi.
Kwa upande wake Wakili Mkuu wa serikali ,Dkt.Ally Posi amesema kuwa ,mafunzo haya ni mwendelezo wa dhamira ya Ofisi yao ya kuwajengea uwezo Mawakali wa serikali wote kutoka wizara ,ofisi,Taasisi na mashirika mbalimbali nchini .
Amesema kuwa, tangu mwaka 2020 OWMS imekuwa ikiratibu na kuendesha magunzo hayo kila mwaka kwa lengo la kuwanjega uwezo Mawakili wa serikali ,kuimarisha uelewa wao wa mausala mubimu ya kisheria, na kuwandaa vyema katika kutekeleza majukumu yao kama Askari wa kalamu wanaolinda uchumi na maslahi mapana ya Taifa kwa ujumla .
Ameongeza kuwa, mafunzo hayo yanahusisha uwasilishaji wa mada mbalimbali kutoka kwa wataalamu waliobobea katika tansia ya Sheria na taaluma nyingine,sambamba na majadiliano ya kina yatakayowapa washiriki fursa ya lubadilishana uzoefu na uelewa wa masuala ya kitaaluma .
Possi amefafanua kuwa, mafunzo hayo yanaongozwa na kauli mbiu”ubobezi wa kisheria kwa ajili ya kesho ,Teknolojia ,mikakati na Mizania ya maisha kwa Mawakili wa serikali katika kufanikish Bira ya Maendeleo ya Taifa 2050″.
Amefafanua kuwa, mafunzo hayo yametolewa na wakufunzi wabobezi ambao no Majaji wa Mahakama Rufani,Mahakama Kuu na Majaji wastaafu kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania ,watalaamu wa sekta ya Sheria na sekta mbalimbali Kitaifa na Kimataifa, wakufunzi kutoka vyuo vikuu hapa nchini pamoja na watalaamu kutoka OWMS.



