NA DENIS MLOWE IRINGA
ALIYEKUWA mchezaji wa Zamani wa Yanga ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa kampuni ya Alishati Limited ya mjini Iringa, Ally Msigwa ametoa msaada kwa timu ya soka ya wanawake ya Mkwawa Queens inayotarajia kuelekea jijini Mwanza kwa ajili ya michezo ya ligi soka Daraja ya wanawake.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo wenye thamani sh milioni 2 Msigwa alisema kuna ulazima wa jamii kutambua kwamba soka la wanawake linahitaji msaada mkubwa sana kwa sababu ni zaidi ya maisha kwa sasa duniani kutokana kuingiza hela.
Alisema kuwa aliamua kutoa msaada huo baada ya kufatwa na viongozi wa timu hiyo na ambayo awali ilikuwa ligi soka la wanawake kabla ya kushuka na sasa wako daraja la kwanza na kuamua kutoa msaada huo mdogo na kuwaahidi endapo itapanda kupitia kampuni ya Alishati atatoa msaada mkubwa zaidi.
Msigwa alitoa wito kwa jamii kuwekeza kwenye soka la wanawake kwani ni ajira tosha katika jamii na kumtolea mfano binti Clara Luvanga kutoka Pawaga mkoani hapa alivyoweza kupiga hatua katika soka la wanawake.
“Sisi wanamichezo tuna ndoto ya kuonana na Christiano Ronaldo ila Clara yeye wanaonana mara kwa mara kutokana na soka hivyo jamii isaidie soka la wanawake kama ilivyo kwa wanaume”Alisema Ally Msigwa.
Aliongeza kuwa msaada huo wa ‘tracksuit’ kwa wechezaji wote na benchi la ufundi itakuwa chachu ya kuwafanya watambulike kama timu ya wanawake kila wanaposafiri katika michezo ya ligi soka daraja la kwanza la wanawake na ataendelea kuwa karibu na timu hiyo ambayo awali alikuwa mmoja wa makocha
Kwa upande wake mwenyekiti wa timu hiyo Joel Musiba licha ya kushukuru kwa msaada huo alitoa wito kwa jamii kutambua kwamba timu hiyo ni ya jamii nzima na wasiiachiwe viongozi peke yao kwani mafanikio ya timu hiyo ndio mafanikio kwa mkoa wa Iringa.
Alisema kuwa timu inapokuwa inacheza ni fursa kwa mkoa wa Iringa na watu wanaingiza pesa kutokana na wageni wanaokuja hivyo wanapoombwa msaada na kudhamini wajitokeza ili kuweza kuendesha timu kwani ni gharama kubwa sana.
Alisema timu za wanawake zina mahitaji makubwa hivyo kitendo cha Ally Msigwa kuisaidia timu hiyo ni uzalendo mkubwa katika kuamini maendeleo ya soka la wanawake mkoani hapa.



Matukio katika picha