Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamini Mkapa ya jijini Dodoma, Profesa Abel Makubi (wa pili kushoto) na Mwenyekiti wa Shirika la TOKUSHUKAI Medical la Japan, Dkt. Shinichi Higashiue (wa pili kulia) wakionesha hati za makubaliano ya ujenzi wa kituo kikubwa cha kupandikiza figo na utoaji mafunzo kwa madaktari bingwa baada ya kutia saini makubaliano hayo mbele ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye ukumbi wa hoteli ya Westin Osaka Japan, Mei 26, 2025. Wengine kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Cosato Chumi, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Profesa Lugano Kusiluka, Rais wa Hospitali ya Shonan Kamakura, Dkt. Shunzo Kobayashi na kulia ni Mshauri wa Masuala ya Afrika wa Shirika la Tokushukai Medical, Dkt. Milanga Mwanatambwe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Shirika la TOKUSHUKAI Medical la Japan pamoja na viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na viongozi wengine wa Taasisi na vyuo nchini Tanzania na Japan baada ya mazungumzo kwenye hoteli ya Westin Osaka nchini Japan, Mei 26, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa ya jijini Dodoma, Profesa Abel Makubi (kushoto) na Mwenyekiti wa Shirika la TOKUSHUKAI Medical la Japan, Dkt. Shinichi Higashiue (kulia) wakibadilishana hati za makubaliano ya ujenzi wa kituo kikubwa cha kupandikiza figo na utoaji mafunzo kwa madaktari bingwa baada ya kutia saini makubaliano hayo mbele ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye ukumbi wa hoteli ya Westin Osaka Japan, Mei 26, 2025. Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Profesa Lugano Kusiluka (wa pili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji, Rais na Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya Shonan Kamakura, Dkt. Shunzo Kobayashi na wa pili kulia ni Mshauri wa Masuala ya Afrika wa Shirika la Tokushukai Medical, Dkt. Milanga Mwanatambwe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)