Katibu wa Chama cha ACT -Wazalendo Wa Jimbo la Tanga Mohamed Salim Ponda (kushoto) akimkabidhi fomu ya kuomba kuteuliwa kuwa mgombea Ubunge Jimbo la Tanga mwanachama wao John Charles Mboggo (katikati) kulia ni Mwenyekiti wa Wazee Jimbo la Tanga (ACT Wazalendo) Zaharan Mohamed
Na Oscar Assenga, Tanga.
KADA wa Chama Cha ACT –Wazalendo Mkoani Tanga John Charles Mboggo amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa kuwania Ubunge katika Jimbo la Tanga kupitia chama hicho huku akihaidi kuirejesha Tanga ya Viwanda ambayo ni ndoto kubwa ya wananchi wa mkoa huo.
Akizungumza leo na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu hiyo alisema lenbgo la kuchukua fomu ya kuwania Ubunge ni kutaka kuhakikisha anatoa mchango wake katika kurejesha viwanda vya Tanga ambavyo wananchi wamekuwa na kiu navyo.
Alisema kwamba kwa sababu viwanda ni ajira na nguvu kazi ya Tanga wanaongelea kuna vijana asilimia 68 ya vijana wakitumika kwenye viwanda watakuwa na uchumi kwenye Jimbo hilo na Mkoa kwa Ujumla.
“Tanga tunaamini sisi ni watu tunaamini watu wa kuleta maendeleo na ndio maana tunawahamasisha wananchi wenye sifa za kupiga kura kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye zoezi la kura kwa lengo la kuwachaguoa viongozi watakaowaongoza”Alisema
Aidha alisema kwamba wasione aibu kutokana na uwepo wa hila mbalimbali wanajua namna ya kubaliana nayo ili kuhakikisha hazijitokezi kwenye mchakato huo.
Awali akizungumza Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Jimbo la Tanga Anasi Mohamed Rweymamu alisema kwamba wanaendelea kuwakaribisha wagombe na kura zao wa maoni ndani ya chama ndizo zitakazoamua nani anaweza kupeperusha tiketi ya chama hicho kwenye nafasi ya Ubunge.
Alisema kwamba ACT Wazalendo ndio chama pekee ambacho kinaweza kupeperusha vyema Bendera yake katika kuibuka na ushindi kwenye nafasi ya Ubunge Jimbo la Tanga na Tanzania kwa upekee.
Naye kwa upande Katibu wa ACT WaaJimbo la Tanga Mohamed Salim Ponda alisema kwamba wapo kwenye maandalizi ya uchaguzi kama chama hicho Taifa kilipotangaza kwamba zoezi la kuchukua fomu kutoka Aprili 18 mwaka huu mpaka 31 mwezi Mei katika nafasi za Ubunge na Udiwani.
Alisema kwamba katika uchaguzi huo wamejipanga kwamba wagombea watakao wapitisha katika kinyang’anyiro cha Ubunge katika Jimbo hilo watakuwa imara kuhakikisha wanapeperusha vyema bendera hiyo.