NA DENIS MLOWE
KAMATI ya mashindano ya Kombe la VunjaBei imetaja timu zilizoingia 25 bora sambamba na timu 7 zilizofanikiwa kuingia kama best looser katika mashindano hayo yaliyojizoelea umaafuru kutokana zawadi kubwa kutolewa tangu kuanzishwa mashindano mbalimbali mkoani Iringa.
Akitaja timu hizo Mwenyekiti wa Kamati wa mashindano hayo yanayodhaminiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Vunjabei Bei, Fred Ngajilo maarufu kama Fred Vunjabei, Pastor Kwambiana alizitaja timu hizo kuwa ni Mgela FC, Spana fc, Super Eagles fc,Isakalilo FC, Walimu fc, Lumuli Fc na Magulilwa FC.
Nyingine ni Viwengi fc, Scout fc, St. Dominic Savio fc, Izazi Fc. Tanesco fc ,
Migori fc, Frelimo na BBC fc.
Kwambiana aliongeza kuwa timu nyingine ni timu za Mti Pesa, Mgama, Mseke , Ifunda Comabine, Nzihi , Kihanga fc Wasa na Kidamali.
Kwa upande wake Katibu wa mashindano ya Kombe la VunjaBei, Yahaya Mpelembwa alisema kuwa baada ya kumaliza raundi ya mtoano na kupata timu 25 bora kamati imekaa na kupitia mwenendo wa ligi na moja ni kuangalia timu zilizoingia kama best looser na taja sababu ambazo timu hizo zimefuzu kwenye hatua hiyo na kuungana na timu 25.
Mpelembwa alisema kuzipata timu hizo walitumia ni timu 25 zilizoshinda moja kwa moja bila kuwa na dosari yoyote ya kikanuni, timu zenye nafasi kuzidi nyingine ikiongozwa na nidhamu ya timu.
Alisema kuwa timu yenye nafasi kuzidi nyingine ikiongozwa na nidhamu ya mashabiki wao ,timu yenye kuongozwa na amani,utulivu na usalama wa viwanja vyao .
Aliongeza kuwa timu yenye nafasi ni ile ambayo mashabiki wao hawana vurugu viwanjani, nidhamu kubwa katika mashindano yote.
Alizitaja timu zilizofanikiwa kuingia katika hatua ya 25 bora kama best looser kuwa ni timu za Kalenga fc, Kising’a Fc, Luhota Fc, Renjaz Fc, Sadan fc , Wakili fc na Morning fighter



