Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Stanslaus Nyongo (Mb,) amesema kuwa Serikali itaendelea kukaa na Wafanyabiashara na Wawekezaji nchini kujadiliana namna bora ya kutatua changamoto za wafanyabiashara ili kuongeza wigo wa ukusanyaji wa kodi.
Mhe. Nyongo ameyasema hayo aliposhiriki mdahalo katika Kongamano la Kodi na Uwekezaji lililofanyika JNICC – Dar es salaam.
Mhe. Nyongo ameongeza kuwa sekta binafsi ndio mhimili wa uchumi wa nchi hii hivyo serikali itaendelea kushirikiana nao ili kukuza uchumi.
Mhe. Nyongo ameongeza kuwa kuanzishwa kwa Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwelezaji (MKUMBI) ulilenga kuondoa tozo na kuboresha sera na sheria na kuunganisha Taasisi za udhibiti ili kutatua changamoto za Biashara kwa wawekezaji.