Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akifanya kikao na viongozi kutoka Hospitali za moyo za nchini Zambia, Rwanda, Uganda pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Save a Child’s Heart la nchini Israel Simon Fisher wakati wa mkutano wa tatu wa kimataifa wa magonjwa ya moyo unaofanyika katika hoteli ya Sea Clif iliyopo mjini Zanzibar
Meneja wa kampuni ya usambazaji dawa za binadamu ya Sun Pharma Abhishek Gahlot akimuelezea bidhaa zinazopatika katika kampuni hiyo Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Moyo ya nchini Zambia Chabwela Shumba alipotembelea banda la kampuni hiyo wakati wa mkutano wa tatu wa kimataifa wa magonjwa ya moyo unaofanyika katika hoteli ya Sea Clif iliyopo mjini Zanzibar
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka nchini India Parag Patel akiwafundisha wataalamu wa magonjwa ya moyo kutoka nchi mbalimbali namna ya kugundua magonjwa mbalimbali ya moyo wakati wa mkutano wa tatu wa kimataifa wa magonjwa ya moyo unaofanyika katika hoteli ya Sea Clif iliyopo mjini Zanzibar
Wataalamu wa magonjwa ya moyo kutoka nchi mbalimbali duniani wakifuatilia mada zinazotolewa katika mkutano wa tatu wa kimataifa wa magonjwa ya moyo unaofanyika katika hoteli ya Sea Clif iliyopo mjini Zanzibar
Picha na: JKCI