Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kushiriki mbio za hisani za Bunge zilizoanzia na kuishia kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Aprili 12, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri mkuu)
……
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewahakikishia Watanzania fedha zilizokusanywa katika mbio za hisani za Bunge zitakwenda kutumika kama ilivyokusudiwa.
Ameyasema hayo leo (Jumamosi, Aprili 12, 2025) katika mbio za hisani za Bunge zilizolenga kuchangisha fedha za ujenzi wa Shule ya Sekondari Bunge Wavulana.
Ujenzi wa shule hiyo shule hiyo itakayokuwa na uwezo wa kusajili wanafunzi wasiopungua 300 hadi 350 kwa mwaka utagharimu zaidi ya shilingi bilioni tatu.
Shule hiyo ya kidato cha tano na sita itajengwa katika eneo la Kikombo, Jijini Dodoma karibu kidogo na shule ya wasichana iliyojengwa na wabunge wanawake 2020.
“Ninawapongeza sana Wabunge wenzangu kwa kuweka alama na kugusa maisha ya Watanzania na watoto wetu wa kiume watakaopata fursa ya kusoma katika shule hiyo.”
Amesema ujenzi wa shule hiyo ni mpango wa Bunge wa kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia suluhu Hassan katika kukuza na kuendeleza sekta ya elimu.
Shule hiyo ya bweni itakuwa maabara nne za biolojia, kemia, fizikia na jiografia, maktaba, bwalo la chakula, nyumba za walimu pamoja na viwanja vya michezo.
Kwa upande wake, Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson amewashukuru washiriki wote wa mbio hizo kwa kuwaunga mkono, Bunge limeonesha mfano wa kujali watoto wote.
Awali, Mwenyekiti wa Mbio za Hisani za Bunge, Festo Sanga alisema lengo la mbio hizo ni kukusanya fedha za ujenzi wa shule ya wavulana. Mbio hizo zilihusisha watu zaidi ya 4,000.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki katika mbio za hisani za Bunge zilizoanzia na kuishia kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Aprili 12, 2025. Kulia kwake ni Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu na kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya washiriki wa mbio za hisani za Bunge zilizoanzia na kuishia kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Aprili 12, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kushiriki mbio za hisani za Bunge zilizoanzia na kuishia kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Aprili 12, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi ya shilingi milioni 5, Boay Dawi baada ya kuibuka mshindi wa kwanza wa mbio za kilomita 21 kwa upande wa wanaume katika mbio za hisani za Bunge zilizoanzia na kuishia kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Aprili 12, 2025. Kushoto ni Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa mbio za hisani za Bunge zilizoanzia na kuishia kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Aprili 12, 2025. Kulia kwake ni Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Taifa, Mary Chatanda katika mbio za hisani za Bunge zilizoanzia na kuishia kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Aprili 12, 2025. Wa tatu kushoto ni Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson Mwansasu na wa pili kushoto ni Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mgeni Hassan Juma. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)