WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe.Mohamed Mchengerwa, akizungumza Leo Aprili 9,2025 wakati akifunga mkutano wa mwaka wa Waganga hao ngazi ya afya ya msingi uliofanyika jijini Dodoma.
SEHEMU ya Washiriki wasikiliza hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe.Mohamed Mchengerwa, (hayupo Pichani) wakati akifunga mkutano wa mwaka wa Waganga hao ngazi ya afya ya msingi uliofanyika jijini Dodoma.
SEHEMU ya Washiriki wasikiliza hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe.Mohamed Mchengerwa, (hayupo Pichani) wakati akifunga mkutano wa mwaka wa Waganga hao ngazi ya afya ya msingi uliofanyika jijini Dodoma
Na.Alex Sonna _DODOMA
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe.Mohamed Mchengerwa,amesema ndani ya miaka minne serikali imeajiri wataalamu wa afya 25,920 wa kada mbalimbali za afya na itaendelea kutoa vibali vya ajira kila mwaka ili kupunguza uhaba ulipo.
Waziri Mchengerwa ameyasema hayo Leo Aprili 9,2025 wakati akifunga mkutano wa mwaka wa Waganga hao ngazi ya afya ya msingi uliofanyika jijini Dodoma.
“Nielekeze Mamlaka za serikali za mitaa kuendelea kutumia fursa ya kuajiri watumishi kwa njia ya mikataba ili kupunguza pengo lililopo la watumishi kwenye maeneo yenu,”amesema Mhe.Mchengerwa
Aidha Mhe.amewaagiza Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wasiwaondoe kwenye nafasi zao Waganga Wafawidhi bila kupima utendaji wao na mwenendo wao wa kiutumishi.
“Nina waelekeza Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Waganga Wafawidhi wasiondolewe kwenye nafasi zao hadi taratibu za kupima utendaji wao na iwapo kutabainika kuna changamoto za kinidhamu au nyingine kubwa zinazosababisha kuondolewa kwenye nafasi zao si kwa utashi wa Mkurugenzi, ninawataka watumie vigezo vya utendaji au upimaji wa ubora si kwa utashi wa Mkurugenzi wa Halmashauri,”amesisitiza
Hata hivyo ametaka Waganga hao kwenda kuimarisha ubora wa huduma za afya, ustawi wa jamii na lishe ikiwa ni nguzo ya kufanikisha mpango wa bima ya afya kwa wote .
“Kila mmoja ahakikishe kituo chake kinafunga na kutumia kikamilifu mfumo wa kielektroniki ulioboreshwa wa afya ifikapo Juni 30 mwaka huu. Jambo jingine kupitia usimamizi shirikishi na ufuatilia mbalimbali tumebaini baadhi ya vituo vinakusanya fedha na kuzitumia kabla ya kupeleka benki na kupeleka fedha pungufu suala hili halikubaliki,”ameaema
Pia amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri kusimamia kwa karibu mapato na matumizi ya fedha za vituo vya kutolea huduma za afya kwa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kuhakikisha kunakuwa na uwazi na matumizi sahihi na kwa wakati wa fedha zinazokusanywa.
Kwa upande wake Waziri wa Afya, Jenista Mhagama amesema serikali ya Rais Samia imefanya uwekezaji mkubwa katika sekta za afya na kuwataka waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma ya afya ngazi ya msingi na watumishi wa sekta hiyo kutekeleza majukumu yao na kusimamia viapo vyao.
Naye Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Grace Magembe amesema kuwa wanganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za afyamsingi ni jeshi kubwa kwa kuwa asilimia 85 ya watanzania wanapata huduma kwenye vituo hivyo.