WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Aprili 7, 2025 ameshiriki Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Miaka 53 ya kifo cha Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume kwenye Afisi Kuu ya CCM Kisiwandua Zanzibar.
Viongozi wengine aliohudhuria ni pamoja na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Stephen Wasira, Mjane wa Hayati Karume, Mama Futuma Karume, Watoto ya Hayati Karume, Amani Abedi Karume na Balozi, Ali Abeid Karume, Rais Mstaafu wa Zanzibar, Ali Mohamed Shein.