Mwenyekiti wa Kamati ya ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Joseph Mhagama akizungumza na baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa sita, ofisi za Walimu pamoja matundu 12 ya vyoo katika Shule ya Sekondari Magila iliyopo katika Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga zinazojengwa na TASAF.
Na Lusungu Helela – MUHEZA
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imesema imeridhishwa na uwekezaji wa miundombinu ya elimu inayoendelea kutekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Mikoa ya Tanga na Pwani huku ikisema miradi hiyo iliyoibuliwa ni hitaji kubwa la wananchi katika Mikoa hiyo.
Amesema TASAF mbali ya kutoa fedha kwa Walengwa, imeanza kujipambanua kwa kuibua miradi ya maendeleo ya elimu ambayo imekuwa msaada mkubwa kwa watoto ambao wengi wao walikuwa wakikatiza masomo kutokana na kukosekana kwa miundombinu hiyo.
Kamati hiyo, imetoa pongezi hizo kwa nyakati tofauti baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa sita, ofisi za Walimu pamoja matundu 12 ya vyoo katika Shule ya Sekondari Magila iliyopo katika Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga pamoja na Shule ya Sekondari Mwavi iliyopo Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani zinazojengwa na TASAF.
Madarasa hayo ya kisasa yatasaidia kuwafanya wanafunzi wa maeneo hayo kusoma kwa bidii katika mazingira mazuri na rafiki hali itakayochangia kuongezeka kwa kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi katika shule hizo.
Akizungumza leo kwa niaba ya Kamati hiyo mara baada ya kutembelea miradi hiyo, Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Dkt. Joseph Mhagama amesema, ujenzi wa miundombinu hiyo ya elimu ni kielelezo na dhamira ya dhati ya Serikali ya kuhakikisha wanafunzi wanatimiza ndoto zao kwa kupata elimu bora ili kutokomeza umaskini katika jamii
“Tunaipongeza Ofisi ya Rais, menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa usimamizi mzuri wa miradi mbalimbali iliyo chini ya Ofisi hiyo kwani tunaona kazi nzuri zinazofanywa na taasisi hizo, tumejionea miradi ya TASAF ilivyotekelezwa kwa viwango na ubora wa hali ya juu, miradi ya aina hii ni muhimu sana kwani inachochea ari ya kusoma kwa wanafunzi wetu,” Mhe. Mhagama alisisitiza.
Tumeona ni miradi inayoleta tija na imetekelezwa kwa ubora na thamani ya fedha imeonekana, hii ni kazi nzuri ambayo Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweza kuifanya kupitia TASAF lakini pia kwa usimamizi mzuri na wananchi wa maeneo husika ” ameongeza.
Kwa upande wake, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu, amesema utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa miundombinu ya utoaji huduma za kijamii unaofanywa na TASAF unalenga kusogeza huduma za kijamii karibu na wanachi pamoja na kuboresha huduma hizo.
TASAF imeweza kujenga shule, madarasa, vituo vya afya, zahanati, madaraja, barabara pamoja na miundombinu ya maji na umwagiliaji, hii yote ni kutaka kuboresha upatikanaji wa huduma za kijamii kama ambavyo Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa akisisitiza mara kwa mara.” amesema Mhe.Sangu
Akizungumzia ujenzi wa shule katika Kijiji cha Mwavi Wilayani Bagamoyo, Mhe. Sangu amesema kukosekana kwa shule katika eneo hilo kulipelekea wanafunzi kutembea umbali mrefu na kushindwa kuhudhuria shule kupindi cha mvua lakini TASAF itakuwa mkombozi kwa watoto hao kwa kuwa karibu na shule hali itakayosababisha mahudhurio na ufaulu kuwa mzuri tofauti na ilivyokuwa mwanzo.
Mbali na hilo, Mhe. Sangu amesema Kamati imejionea na imeridhika na thamani halisi ya fedha ya ujenzi miundombinu katika Shule ya Sekondari Magila na hivyo kuwafanya watoto hao kusoma shule katika mazingira mazuri na rafiki kwa ajili ya mustakabali ya maisha yao ya badae.
“Kamati imejionea baadhi ya majengo ambayo yamechakaa sana yaliyojengwa tangu mwaka 1932 ambayo ni hatarishi na yenye mazingira magumu kwa wanafunzi kusoma kwa bidii lakini TASAF imebadilisha hata mandhari ya eneo hili kwani miundombinu iliyopo inavutia na kuwafanya wanafunzi kusoma kwa bidii’’ amesisitiza Mhe. Sangu
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imekagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Mikoa ya Pwani na Tanga ambapo kesho itaendelea na ziara hiyo katika Mkoa wa Kilimanjaro kukagua miradi ya TASAF na TAKUKURU.
Mwenyekiti wa Kamati ya ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Joseph Mhagama akizungumza na baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa sita, ofisi za Walimu pamoja matundu 12 ya vyoo katika Shule ya Sekondari Magila iliyopo katika Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga zinazojengwa na TASAF.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akizungumza na baada ya Wajumbe wa Kamati ya ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheriakutembelea na kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa sita, ofisi za Walimu pamoja matundu 12 ya vyookatika Shule ya Sekondari Magila iliyopo katika Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga zinazojengwa na TASAF.
Mwenyekiti wa Kamati ya ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Joseph Mhagama akiwa ameongozana na baadhi ya ya Wajumbe wa Kamati ya ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria akisalimiana na baadhi ya viongozibaada ya kuwasili kwa ajili ya kutembelea na kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa sita, ofisi za Walimu pamoja matundu 12 ya vyoo katika Shule ya Sekondari Magila iliyopo katika Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga zinazojengwa na TASAF.
Mwenyekiti wa Kamati ya ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Joseph Mhagama akiwa ameongozana na baadhi ya ya Wajumbe wa Kamati ya ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheriabaada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa sita, ofisi za Walimu pamoja matundu 12 ya vyoo katika Shule ya Sekondari Magila iliyopo katika Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga zinazojengwa na TASAF.
Muonekano wa madarasa yaliyojengwa katika shule ya Sekondari ya Magila kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) iliyopo katika Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga.
Muonekano wa jengo la utawala lililojengwa katika shule ya Sekondari ya Magila kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) iliyopo katika Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga