Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wagonja wa nje katika Kituo cha Afya Itobo kilichopo Jimbo la Bukene wilayani Nzega wakati alipokagua upanuzi wa kituo hicho, Machi 13, 2025. Kulia kwake ni Mganga Mfawidhi wa kituo hicho, Dkt. Siraji Yusufu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozwa na Dkt. Siraji Yusufu ambaye ni Mfawidhi wa Kituo cha Afya Itobo katika Jimbo la Bukene wilayani Nzega (wa pili kushoto) kukagua upanuzi wa kituo hicho, Machi 13, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimjulia hali Rehema Hamis aliyelazwa kwenye Wodi ya Wazazi katika Kituo cha Afya Itobo kilichopo Jimbo la Bukene wilayani Nzega akisubiri kujifungua. Mheshimiwa Waziri Mkuu alikwenda kukagua upanuzi wa kituo hicho Machi 13, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Muonekano wa jengo la kitengo cha mionzi katika Kituo cha Afya Itobo kwenye Jimbo la Bukene wilayani Nzega ambacho Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua upanuzi wake, Machi 13, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)