NA DENIS MLOWE IRINGA
KAMATI ya maandalizi ya mashindano ya ligi kugombea kombe la Vunjabei wametoa elimu kwa viongozi na manahodha wa timu 50 zitakazoshiriki mashindano hayo yanayotarajia kuanza hivi karibuni.
Mafunzo hayo yametolewa kwa viongozi hao na wawezeshaji mbalimbali wakiongozwa na Mwenyekiti wa Mashindano hayo Yahaya Mpelembwa akiambatana na wataalam wa afya, usalama.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika uwanja wa Samora, mmoja ya wawezeshaji katika suala la Afya Dr. Kenny Edwin alisema timu zitumie wataalam wa afya na kuacha kutumia watu ambao hawana taalum ya kutibu wachezaji inaweza kusababisha madhara zaidi kwa mchezaji.
Alisema kuwa elimu inayotolewa kwenye mashindano ya Kombe la Vunja Bei linalodhaminiwa na mfanyabiashara maarufu nchini Fred Ngajilo kuhakikisha kuwe na barafu, Dawa za kuchua, clip bandage, Glovu na dawa ya muhimu sana kwa mchezaji ambayo ni spray ya Deep Hit na ayodini kwa ajili ya kukausha damu.
Aidha alitoa wito kwa viongozi wa timu kuwapima afya wachezaji ambao watashiriki mashindano hayo na kuongeza kuwa kama sio kuwapima wafanye maongezi na wachezaji kwa lengo la kuwajenga kisaikolojia katika kupunguza presha kabla ya mchezo.
Kwa upande wake mwezeshaji katika upande wa Usalama Pastory Kwambiana alisema kuwa mashabiki ambao watakuja viwanjani kuacha kuvuta bangi au madawa ya kulevya katika viwanja vya soka kwa kuwa vina madhara makubwa kwao na kwa wachezaji.
Alisema hawatasita kumkamata mtu au kikundi ambacho kitajihusisha kuharibu hali ya hewa ya uwanja kwa kutumia vilevyi ambavyo havitakiwi viwanjani ikiwemo mambo ya ulozi.
Kwa Upande wake, mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF Abuu Silia akizungumza katika semina hiyo alizitaka timu shiriki kuhakikisha wanazingatia idadi ya ya watu wanaokaa katika benchi la ufundi kuliko timu iwe na watu wengi bila kuzingatia idadi.
Abuu ambaye pia ni kamishna wa ligi kuu Tanzania Bara alisema kuwa benchi la ufundi linatakiwa kuwa na idadi ya watu 10 na wachezaji na kutoa wito kwa waandaji kuandaa benchi la ufundi ambalo litakuwa na watu sahihi.
Alisema kuwa kocha mkuu ndio msimamizi wa benchi la ufundi hivyo jambo lolote ambalo litakuwa kinyume na sheria na kanuni litakuwa linavunja sheria za soka.
Silia alisema kuwa katika mpira wa miguu suala la nidhamu ni la muhimu sana na endapo timu au mchezaji anaweza sababisha adhabu kwa mchezaji husika au timu husika.
Naye Katibu wa Mashindano hayo Yahaya Mpelembwa alizitaja timu ambazo zitashiriki mashindano hayo baada ya mchujo mkali ulioshirikisha timu zaidi ya 130 kuwa ni Mti pesa , Wasa FC ,Migoli FC, Izazi kids , Walimu Fc , Mseke FC, Muwimbi fc, Morning fighter, Fox FC
Nyingine ni Magunga FC, Kimande Fc, Magic site FC, City center FC , Kihanga Fc, Kihesa FC, Igangidungu FC , Dream boyz FC, Isakalilo FC , Mgama FC, Spana Fc, .Scout FC, Kidamali fc, St.Dominic Fc,, Nzihi Fc na Kalenga FC
Aliongeza kuwa washiriki wengine wa mashindano hayo ni timu za Kitwiru FC Magunga FC , Suma Jkt FC ,Magulilwa FC
,Mbugani FC ,Rucu Metro FC, BBC Foundation, Ilolo united, Sadan fc, Fema FC, Ifunda combine, Flerimo FC ,Super eagle, Wakili Fc, Kitwiru FC, Kihesa FC



