Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza kwenye fainali za mashindano ya 16 ya kuhifadhi Qur’an Tukufu ngazi ya Afrika ya Mashariki na Kati yaliyofanyika kwenye Uwanja wa mpira wa miguu wa Azam uliopo Chamazi jijini Dar es salaam, Machi 8, 2025. Mashindano hayo yaliandaliwa na Taasisi ya Manah’ilal al Irfan. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Mdhamini wa Taasisi ya Manah’ilal al Irfan, Sheik Alhad Mussa Salum kuingia kwenye uwanja wa mpira wa miguu wa Azam uliopo Chamanzi jijini Dar es Salaam kuwa mgeni rasmi katika fainali za mashindano ya 16 kuhifadhi Qur’an Tukufu ngazi ya Afrika ya Mashariki na Kati, Machi 8, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi alipowasili kwenye uwanja wa mpira wa miguu wa Azam uliopo Chamazi jijini Dar es salaam kuwa mgeni rasmi katika fainali za mashindano ya kuhifadhi Qur’an Tukufu ya Afrika ya Mashariki na Kati, Machi 8, 2025. Mashindano hayo yaliandaliwa na Taasisi ya Manah’ilal al Irfan Foundation. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akimpongeza Ali Juma Bakari, mshindi wa kwanza wa fainali za mashindano ya 16 ya kuhifadhi Qur’an Tukufu ngazi ya Afrika ya Mashariki na Kati yaliyofanyika kwenye Uwanja wa mpira wa miguu wa Azam uliopo Chamanzi jijini Dar es Salaam, Machi 8, 2025. Kushoto ni Sheikh Alhad Mussa Salum.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikabidhiwa tuzo maalum na Sheikh Alhad Mussa Salum ambaye ni Mdhamini wa Taasisi ya Manah’ilal al Irfan iliyoandaa mashindano ya 16 ya kuhifadhi Qur’an Tukufu ya Afrika ya Mashariki na Kati yaliyofanyika Kwenye Uwanja wa mpira wa miguu wa Azam uliopo Chamanzi jijini Dar es salaam, Machi 8, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika fainali za mashindano ya 16 ya kuhifadhi Qur’an Tukufu ngazi ya Afrika ya Mashariki na Kati yaliyofanyika wakimsikiliza mgeni rasmi, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipozungumza kwenye Uwanja wa mpira wa miguu wa Azam uliopo Chamanzi jijini Dar es salaam, Machi 8, 2025. Mashindano hayo yaliandaliwa na Taasisi ya Manah’ilal al Irfan. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na viongozi wakiwa katika picha ya pamoja na washirki wa fainali za mashindano ya 16 ya kuhifadhi Qur’an Tukufu ngazi ya Afrika ya Mashariki na Kati, Machi 8, 2025. Mashindano hayo yaliandaliwa na Taasisi ya Manah’ilal al Irfan. Kushoto kwake ni Mdhamini wa Taasisis hayo, Sheikh Alhad Mussa Salum.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
….
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema vijana wenye elimu na maarifa ya dini ni nguzo muhimu ya ustawi na maendeleo katika jamii kwani imani imara ya kidini hujenga jamii zenye maadili mema, ufanisi katika kazi, na upendo wa dhati kwa kila mmoja.
Pia, Mheshimiwa Majaliwa amesema Serikali ina matarajio makubwa kwa vijana wanaoshiriki mashindano Quran kwani kwa kutumia maarifa na ujuzi wanaoupata katika mashindano hayo kutekeleza majukumu muhimu ya kijamii na kiroho.
Ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Machi 8, 2025) alipozungumza na wananchi katika Mashindano ya 16 ya Kuhifadhi Quran Tukufu ngazi ya Afrika Mashariki na Kati yaliyofanyika katika uwanja wa Azam Complex Chamanzi, Dar es Salaam.
“Mashindano haya ni fursa ya kukuza imani na maarifa yenu. Kuhifadhi Quran ni jambo lenye manufaa mengi kwani inaimarisha uhusiano wenu na Mwenyezi Mungu na inajenga msimamo wa kiroho. Nina hakika mnapokuwa na imani imara, nidhamu, na maadili mazuri baadaye mtakuwa viongozi bora wa familia, jamii, na Taifa kwa ujumla.”
Waziri Mkuu ameongeza kuwa mashindano hayo yana mchango mkubwa katika kuimarisha amani, mshikamano na utulivu wa nchi, pia yanachangia katika kukuza sekta mbalimbali ikiwemo ya uchumi na utalii kwani kila mwaka washiriki kutoka mataifa mbalimbali wanakuja nchini kushiriki au kushuhudia mshindano hayo.
Akizungumzia kuhusu umuhimu wa mashindano ya kuhifadhi Quran, Waziri Mkuu amesema mashindano hayo yana manufaa kwa washiriki na kwa Taifa kwani yanawawezesha washiriki kuwa na uwezo wa kuhifadhi na kuelewa mafundisho ya Quran Tukufu. “Kupitia mashindano haya, tunawahamasisha vijana wetu kuwa na moyo wa kumtumikia Mwenyezi Mungu kwa juhudi kubwa.”
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa ametumia fursa hiyo kuipongeza taasisi ya Mana’Hil AL – Irfan kwa juhudi zao kubwa katika kuandaa mashindano hayo. “Uwezo wa kuwa na mashindano haya kwa miaka 16 mfululizo ni dalili ya dhamira thabiti ya kuwahamasisha vijana wetu katika kuzingatia na kuhifadhi Quran Tukufu na kuhakikisha kwamba tunalinda utamaduni wa dini, maadili na imani ya Kiislamu.”
Kadhalika, Waziri Mkuu amesema kwamba Serikali inaunga mkono taasisi zote zinazojitahidi kuinua elimu ya dini na maadili, kwa lengo la kuwa na Taifa lenye vijana bora, wenye imani thabiti na maadili mema.
Pia, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa viongozi dini waendelee kuliweka suala la kudhibiti mmomonyoko wa maadili kuwa ajenda ya kudumu katika vikao na mikutano yao.“Ninawasihi sana endeleeni kukemea vikali vitendo vyote ambavyo vinamchukiza Mwenyezi Mungu na ni kinyume na maadili ya dini na utamaduni wa Mtanzania.”