Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongoza matembezi ya hisani yaliyoandaliwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwa ajili ya kuadhimisha miaka 50 ya Taasisi hiyo. Matembezi hayo yameanzia Ofisi za taasisi hiyo iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam, Machi 07, 2025. Matembezi hayo yanalengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuchapa na kusambaza Vitabu vya Kiada kufikia uwiano wa kitabu kimoja, mwanafunzi mmoja. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………….
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TET) inaadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake kwa kuendesha matembezi ya hisani, tukio lililoongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, leo (Ijumaa, Machi 7, 2025) katika ofisi za TET, Mikocheni, Dar es Salaam.
Katika hotuba yake, Waziri Mkuu amesisitiza umuhimu wa upatikanaji wa vitabu shuleni, akihimiza TET kuongeza wigo wa kushirikiana na wadau wa sekta binafsi na kampuni za uchapishaji ili kufanikisha kampeni ya Kitabu Kimoja kwa Mwanafunzi Mmoja.
“TET imeonesha dhamira ya dhati kuchapisha vitabu kwa wingi ili kuhakikisha uwiano wa kitabu kimoja kwa mwanafunzi mmoja, hatua itakayochangia kuboresha elimu nchini,” alisema Majaliwa, huku akimpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mageuzi makubwa katika sekta ya elimu.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dkt. Aneth Komba, alisema kampeni hiyo inalenga kukusanya shilingi bilioni 297 kwa ajili ya kuchapisha vitabu na kununua kompyuta za kuhifadhi vitabu. Kampeni hiyo inatarajiwa kufikia kilele chake Juni mwaka huu.
Kupitia ushirikiano wa sekta binafsi na jamii, TET inalenga kuhakikisha kila mwanafunzi nchini anapata kitabu kimoja, hatua inayowiana na malengo ya kitaifa ya elimu bora na maendeleo endelevu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongoza matembezi ya hisani yaliyoandaliwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwa ajili ya kuadhimisha miaka 50 ya Taasisi hiyo. Matembezi hayo yameanzia Ofisi za taasisi hiyo iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam, Machi 07, 2025. Matembezi hayo yanalengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuchapa na kusambaza Vitabu vya Kiada kufikia uwiano wa kitabu kimoja, mwanafunzi mmoja. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipiga makofi baada ya kukata utepe na kuzindua kampeni maalum ya MWANAFUNZI MMOJA, KITABU KIMOJA yenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuchapa na kusambaza vitabu vya kiada kufikia uwiano wa kitabu kimoja, mwanafunzi mmoja., Mikocheni Jijini Dar es Salaam , Machi 07, 2025. Kushoto ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Omari Kipanga, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania Dkt. Aneth Komba, Mwenyekiti wa Baraza la TET Prof. Maulid Mwatawala. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda wakiwa wameshika bango lenye kampeni maalum ya MWANAFUNZI MMOJA, KITABU KIMOJA yenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuchapa na kusambaza vitabu vya kiada kufikia uwiano wa kitabu kimoja, mwanafunzi mmoja, Mikocheni Jijini Dar es Salaam , Machi 07, 2025.Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Omari Kipanga, na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania Dkt. Aneth Komba, Mwenyekiti wa Baraza la TET Prof. Maulid Mwatawala. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kuongoza matembezi ya hisani yaliyoandaliwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwa ajili ya kuadhimisha miaka 50 ya Taasisi hiyo, Mikocheni jijini Dar es Salaam, Machi 07, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)