KUELEKEA Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani, Wanawake kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania wametembelea Kituo cha Wasioona Watu Wazima kilichopo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma na kutoa msaada wa mahitaji mbalimbali.


Akizungumza mara baada ya kufika katika kituo hicho,Naibu katibu Mkuu Tume ya kurekebisha sheria Bi. Zainabu Chanz amesema

Bi.Zainabu amesema kuwa katika kipindi hiki cha kuelekea maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani, wanawake wa wanakumbushwa kutimiza wajibu wao kwa jamii kama wazazi kwa ustawi wa jamii yetu.


“Wao kama wakinamama wameona ni vyema kuadhimisha siku hiyo kwa kutoa misaada mbalimbali kwa wahitaji hao ikiwemo Mchele Kg100, Maharage Kg100, Mipira ya kumwagilia maji 2, Unga sembe Kg100, Chumvi Pisi 80, Mafuta ya kula Lita 40, Sabuni za Unga mifuko 2 sawa na pisi 60″amesema
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kituo hicho Mzee Yaledi Chereso amesema kuwa kituo hicho wanaishi kwa kujitegemea wenyewe na misaada kutoka wa wadau mbalimbali hivyo kwa ujio wao umeleta matumaini ma faraja katika kituo hivyo

Aidha Mzee Chereso ametoa ombi kwa tume hiyo kuwapatia elimu ya sheria kutoka kwa wataalamu hao ili kujua haki zao za msingi kama walemavu kwani kwakufanya hivyo kutaleta mshikamano na kupinga ukatiki wa kijinsi
Naye Mmoja wa wanaoishi katika kituo hicho Vumilia Sara Mgandu,ameeleza kuwa ingawa anasumbuliwa na ulemavu wa macho lakini anajishughulisha na utengenezaji wa sabuni za maji, kuku na ndizi (Ujasiriamali) hivyo ameshukuru kwa misaada hiyo ikiwemo kumuungisha bidhaa zake.















