
WAZIRI wa katiba na Sheria Dkt.Damas Ndumbaro akisikiliza kero za wananchi mkoani Arusha .

Wananchi mbalimbali waliofika kwenye banda la katiba na Sheria kwa ajili ya kusikilizwa changamoto zao ambapo walikuwa wanahudumiwa na waziri wa katiba na Sheria.
Happy Lazaro,Arusha .
Arusha .WAZIRI wa katiba na Sheria Dkt
Damas Ndumbaro ameagiza kuchukuliwa hatua kwa watumishi wa umma ambao wamekuwa chanzo cha migogoro kwa wananchi ikiweko ya ardhi.
Ameyasema hayo leo mkoani Arusha wakati akisikiliza migogoro ya ardhi kwa wananchi waliofika kwenye banda la katiba na Sheria kwa ajili ya kupata haki zao katika wiki ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani unayotarajia kufanyika machi 8 mwaka huu.
Amesema kuwa, Rais Samia amemtuma kwenda Arusha kwa ajili.ya kushughulikia kero za wananchi huku akimwagiza kimchukulia hatua mtumishi.yoyote wa umma ambaye amekuwa chanzo cha migogoro kwa wananchi ..
“Nimekuja kuweka kambi Arusha pamoja na timu ya wanasheria zaidi ya hamsini kutatua changamoto za wananchi na nikimaliza kuongea na ninyi.hapa naanza kusikiliza mwananchi mmoja mmoja kero yake na kuhakikisha inatatuliwa.”amesema Waziri.
Dokta Ndumbaro amesema kuwa ,Rais Samia amemtuma Arusha kushughulika na migogoro ya wananchi na kuipatia ufumbuzi wa kisheria kwani bado kuna wananchi wengi wanaokabiliana ja changamoto mbalimbali.
Ameongeza kuwa, baadhi ya kero watazimaliza ndani ya siku nane na zile ambazo hazitakwisha wanasheria wataendelea nazo kwa gharama ya Rais Samia .
Amefafanua kuwa, Rias Samia ameagiza mtumishi yoyote anayesababisha migogoro achukuliwa hatua hataka sana iwezekanavyo kwani anasababisha wanacho kuendelea kuwa kwenye migogoro kila wakati badala ya wao kuwa watatuzi wa migogoro hiyo.
Aidha amewataka wananchi wa mkoa wa Arusha kuhakikisha wanatumia fursa hiyo vizuri kupata haki zao kwani huduma imesogezwa karibu yao ili wapate haki zao za msingi.