Shirika lisilokuwa la kiserikali la Nyasa Environment Restoration Iniative (NERI) LA Jijini Dare es salam limekabidhi Zana za uvuvi,Mizinga ya nyuki 20 kwa Kikundi cha Uvuvi cha Dagaa safi katika kijiji Cha Liweta Kata ya Mbaha na pikipiki 1 kwa ajili ya Afisa Uvuvi , Wilaya ya Nyasa.
Mkurugenzi wa Shirika la NERI Bw. Daniel Nkondola amekabidhi vifaa hivyo hivi karibuni katika ofisi za kikundi hicho zilzopo katika Mwalo wa Liweta na kuwataka kutumia vifaa hivyo kwa lengo la kuboresha maisha yao kwa kuwa ni zana bora za uvuvi, kufanya Uvuvi endelelevu na kufanya utnzaji wa mazingira.
Amevitaja vifaa alivyowagawia wanakikundi hao kuwa ni Boti 4 , injini 2 za boti, nyavu za kuvulia dagaa, na chanja za kisasa za kuanikia dagaa, Mizinga ya nyuki, sare kwa ajili ya kikundi na Betri gari 1, na pikipiki moja kwa Afisa Uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa kwa ajili ya kuwezesha usafiri kulea kikundi.
Bw. Nkondola amefafanua kuwa lengo mahsusi ya kugawa vifaa hivyo ni Kuhamasisha Uvuvi endelevu katika kutunza Raslimali za Uvuvi, kuhamasisha utunzaji wa mazingira, kuondoa umaskini na kutunza viumbe vya majini na nchi kavu mategemeo ya Shirika ni kuwajengea uwezo wanakikundi uwezo wa kujiajiri, kupata kipato, uhifadhi wa mazingira na kuondokana na umaskini kwa wananchi wa Wilaya ya Nyasa.
Akipokea Zana hizo kwa niaba yawanakikundi cha dagaa safi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Bw. Khalid Khalif amelipongeza shirika la NERI kwa jitihada katka kukuza sekta ya Uvuvi na kuhamasisha Uvuvi wa kisasa na kutunza mazingira na kutatua changamoto za wanakikundi na ametoa wito kwa shirika hilo kuendeleza ushirikiano.
Kwa upande wao wanakikundi wa kikundi cha Dagaasafi Liweta wamelishukuru shirika hilo kwa Ufadhili na kusema kuwa changamoto zilizokuwa zinawakabili zimetatuliwa hivyo wataendelea kufanya kazi kwa juhudi ili kuboresha hali ya maisha yao.