Mtendaji Mkuu wa Benki ya I&M Zahir Mustafa (katikati), Mkuu wa Kitengo cha Wateja Rejareja Benk ya I&M Simon Gachahi (kushoto) na Mkuu wa Benki za Wateja wa Kibinafsi, Bi Deepali Ramaiya (kulia) wakizungumza na waandishi wa habari leo Machi 3 2025 jijini Dar es salaam kuhusu Kampeni ya ‘NI BURE KABISA’, Inayotoa Uhamisho wa Bure bila Kikomo kutoka Benki hadi Mitandao ya Simu kwa wateja Wake.
Mtendaji Mkuu wa Benki ya I&M Zahir Mustafa akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo,Mhamasishaji Meena Ally Minna Ally wakati wa kutambulisha Kampeni ya ‘NI BURE KABISA’, Inayotoa Uhamisho wa Bure Bila Kikomo kutoka Benki hadi Mitandao ya Simu kwa Wateja Wake Wote.
………….
Benki Benki ya I&M imekuja na suluhisho la kifedha za kibunifu zinazolenga wateja wake kutoa uhamisho wa bure bila kikomo kutoka akaunti za I&M Bank kwenda mitandao ya simu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 3, 2025 jijini Dar es Salaam katika hafla ya uzinduzi rasmi kampeni ya ‘NI BURE KABISA’, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya I&M, Zahid Mustafa, amesema kuwa kampeni hiyo inatoa uhamisho wa fedha bure bila kikomo kutoka akaunti za benki ya I&M kwenda mitandao ya simu, huku akieleza kuwa mpango huu unasisitiza dhamira ya benki ya kuimarisha urahisi wa benki za kidijitali wakati wa kufanya malipo ya gharama nafuu kwa wateja wetu.
“Kupitia ‘NI BURE KABISA’, wateja wa I&M Bank wanaweza kuhamisha fedha kwa urahisi hadi mifumo yote mikubwa ya pesa za simu—M-Pesa, Tigo Pesa (Mixx by Yas), Airtel Money, HaloPesa, na nyinginezo—bila gharama yoyote, na hivyo kuimarisha dhamira ya benki ya kutoa suluhisho za kifedha za kibunifu zinazolenga wateja” amesema Zahid.
Ameongeza kuwa njia ya pesa za simu nchini Tanzania zimekua kwa kasi zaidi kuliko benki za jadi, huku akieleza kuwa upenyezaji wa pesa za simu nchini unakadiriwa kuwa kati ya 70-80% na kuonyesha wateja wa mifumo ya pesa za simu kuongezeka.
Amesema kuwa I&M Bank Tanzania wanaelewa jukumu la msingi pesa za simu limechukua maisha ya kila siku ya wateja jambo ambalo limewafanya kuchukua hatua ya kuwasaidia wateja wao ili kuokoa kwa kuondoa ada za muamala.
Zahid amesema kuwa hivi karibuni wameongeza ujuzi kwa kaweka mkakati wa kuwahudumia wateja wa rejareja pamoja na benki zaidi ya 45 katika soko. “Ada na gharama bado ni changamoto katika sekta ya benki, gharama za uhamisho kutoka benki kwenda mitandao ya simu zinaweza kufikia hadi TZS 12,000 kwa kila muamala, wateja sasa watafurahia akiba kubwa katika miamala yao ya kila siku.”amesema Zahidi
Mkuu wa Sekta ya huduma za Rejareja na Benki za Kidijitali Bw. Simon Gachahi, , amebainisha kuwa upanuzi wa benki katika sekta ya rejareja ulianza na urekebishaji wa benki za kibinafsi, ambapo zimelenga wafanyakazi wanaolipwa mshahara kupitia suluhisho za benki za mahali pa kazi.
“Leo tunawazindua akaunti za moja biashara na zaidi zinazolenga wateja wa SME (wasio na mishahara).”
Akaunti za I&M Biashara zimeundwa kuongeza thamani kwa SMEs na wateja wanaolipwa mshahara kwa kuondoa gharama za juu za uhamisho kutoka benki hadi pochi za simu wakati wa kufanya malipo kupitia njia zetu za kidijitali, mpango huu umeongozwa na maoni ya moja kwa moja ya wateja yaliyokusanywa kupitia mijadala katika miezi michache iliyopita” amesema Simoni.
“Kampeni ya ‘NI BURE KABISA’ imepangwa kuwanufaisha watu binafsi na wafanyabiashara, ikitoa njia rahisi na ya gharama nafuu ya kutuma pesa mara moja kote Tanzania.
Nae Mkuu wa Benki za Wateja wa Kibinafsi, Bi Deepali Ramaiya amesema, “Mbali na faida hizi, wateja wanaweza kupata riba ya hadi 4% kwenye salio la akaunti zao na kufuraishwa na uhamisho wa pesa wa papo hapo kutoka akaunti zao nchini Tanzania, Matawi ya I&M, Kenya, Uganda, na Rwanda. pamoja na mtandao wa zaidi ya Wakala 200 Tanzania.
Mkuu wa Mikopo ya Kidijitali, Masoko na Mawasiliano, Bi Zainab Maalim, amesisitiza kuwa pamoja na mkakati wa kidijitali kampeni hiyo I&M Bank itakuwa kwenye mitaa ya Mkoa wa Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Moshi na maeneo mengine kupitia shughuli zao za Mchakamchaka, wakishirikiana Muhamasishaji Meena Ally ambaye ni Balozi wa benki hiyo katika kuelimisha wateja kuhusu suluhisho la huduma za kifedha na kuwasaidia kufungua akaunti zao.
I&M Bank Limited Tanzania ni benki ya kibiashara nchini Tanzania yenye makao makuu Mkoa wa Dar es Salaam tanzu ya I&M Bank Group yenye makao yake Kenya. Imepokea leseni kutoka Benki kuu ya Tanzania na inafanya kazi kupitia matawi 8 ya I&M Bank Tanzania, ATM na usambazaji wa Wakala.