Baadhi ya Wananchi waliojitokeza kujiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura katika Wilaya ya Magharibi A ,Shehia ya Sharifu Msa kufuatia Zoezi la Uandikishaji Wapiga Kura katika Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Baadhi ya Wananchi waliojitokeza kujiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura katika Wilaya ya Magharibi A ,Shehia ya Kibweni kufuatia Zoezi la Uandikishaji Wapiga Kura katika Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Kamishna wa Tume ya Uchaguzi Idrisa Haji Jecha kizungumza na Mawakala wa Vyama Wakati walipofanya Ziara ya Kutembelea Vituo vya Uandikishaji katika Daftari la Wapiga Kura zoezi lililoanza katika Wilaya ya Magharibi A Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Na Sabiha Khamis Maelezo
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jaji George Joseph Kazi amesema Zoezi la Uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura katika Wilaya ya Magharib A linaendelea vizuri kutokana na ushirikiano uliopo kwa wananchi na waendesha zoezi hilo.
Ameyasema hayo katika kituo cha uandikishaji wa daftari la wapiga kura wapya Mtoni Chemchem alipokuwa akitembelea vituo hivyo katika Wilaya ya Magharib “A”
Amesema kuwa katika Wilaya hiyo muitikio wa wananchi umekuwa mkubwa ambapo vijana wengi waliokuwa hawajapata nafasi ya kuandikishwa wamejitokeza kwa wingi na amani ili kuhakikisha shughuli zote zinakamilika kwa utulivu.
Jaji Kazi, amefafanua kuwa katika Wilaya hiyo wanatarajia kuandikisha watu 12,955 kutokana na Sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2022 ambapo vijana waliofikia umri wa miaka 18 kujiandikisha.
Nae, Mkuu wa Kituo cha Uandikishaji Shehia ya Mtoni Chemchem Ahmada Haji Khamis amesema ,oezi linakwenda vizuri ingawa kuna changamoto za kawaida ambazo zinazoweza kutatulika na kuendelea na zoezi kwa amani na utulivu.
Kwa upande wao wananchi waliojitokeza kujiandikisha wamesema kuwa zoezi hilo linakwenda vizuri kwa utaratibu uliopangwa na kuwaomba vijana wenzao kutumia fursa hiyo muhimu ya kujitokeza kujiandikisha ili kuweza kuchagua kiongozi bora katika uchaguzi mkuu.
Zoezi hilo la uandikishaji katika Wilaya ya Magharibi A litakuwa la siku 3 ambapo jumla ya vituo nane vimetembelewa katika Wilaya hiyo ikiwemo Sharifu Msa, Kibweni, Chemchem, Mwanyanya, Kwa Goa, Mtoni, Mtoni Chemchem na Mtoni Kidatu.