Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza alipomwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Maombi Maalum ya Kuliombea Taifa yaliyoandaliwa na Umoja wa Viongozi wa Makanisa nchini kwenye Viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam, Februari 28, 2025.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
*Atoa wito kwa viongozi wa dini waendelee kuliombea Taifa, viongozi wake
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ametoa wito kwa viongozi wa dini waendelea kuliombea Taifa na viongozi wake kwani pasipo na amani na utulivu nchi haiwezi kutimiza malengo ya kuwaletea Watanzania maendeleo ya kiuchumi.
“Nchi haiwezi kuwa na uhuru wa kuabudu, pasipo amani hatuwezi kufanya shughuli za uzalishaji mali. Katika eneo hili ninawapongeza na kuwashukuru madhehebu yote ya dini kwa kuendelea kuiombea nchi yetu amani, mshikamano na utulivu.”
Waziri Mkuu ametoa wito huo jana usiku (Februari 28, 2025) katika viwanja vya Leaders Club alipomuwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati maombi maalum ya Kitaifa iliyoandaliwa na Umoja wa Viongozi wa Makanisa.
Alisema suala la ushirikiano kati ya Serikali na madhehebu ya dini, limekuwa kipaumbele cha Serikali ya awamu ya sita na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia amekuwa kinara katika hilo.
“Amekuwa akiwashirikisha viongozi wa dini katika masuala mbalimbali, wakati mwingine amefanya nao mazungumzo na anawatembelea. Vitendo hivyo vinadhihirisha jinsi Serikali inavyowathamini viongozi wa madhehebu ya dini.”
Katika ibada hiyo viongozi hao wa Makanisa walitumia fursa hiyo pamoja na mambo mengine kuliombea Taifa lidumishe muungano, amani, utulivu, umoja na mshikamano, pia waliuombea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Alisema kuwa Serikali kwa upande wake imekuwa ikichukua hatua za makusudi za kuinua ustawi wa wananchi wote bila kujali itikadi zao za imani, hizo ni pamoja na utekelezaji wa mipango na mikakati kuhakikisha kuwa wananchi wote wanafikiwa na huduma bora mbalimbali za kijamii.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza alipomwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Maombi Maalum ya Kuliombea Taifa yaliyoandaliwa na Umoja wa Viongozi wa Makanisa nchini kwenye Viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam, Februari 28, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Watanzania wakishiriki katika Maombi Maalum ya Kuliombea Taifa yaliyoandaliwa na Umoja wa Viongozi wa Makanisa nchini kwenye Viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam, Februari 28, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia washiriki wa Maombi Maalum ya Kuliombea Taifa yaliyoandaliwa na Umoja wa Viongozi wa Makanisa nchini kwenye Viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam, Februari 28, 2025. Kushoto ni Mkuu wa Kanisa la Calvary Assemblies of God, Dunstan Maboya. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia washiriki wa Maombi Maalum ya Kuliombea Taifa yaliyoandaliwa na Umoja wa Viongozi wa Makanisa nchini kwenye Viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam, Februari 28, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Cahalamila katika Maombi Maalum ya Kuliombea Taifa yaliyoandaliwa na Umoja wa Viongozi wa Makanisa nchini kwenye Viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam, Februari 28, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)