Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Felcheni Mramba,amesema zaidi ya wananchi 100,000 kutoka vijiji 120 wamenufaika na mradi wa umeme-Songea uliofadhiliwa na Serikali ya Sweden ka thamani ya fedha za Sweden Milioni 700 sawa na shilingi bilioni 169.59 za kitanzania ambao utekelezaji wake ulianzi mwaka 2017 na kuhitimishwa leo.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa Mkutano wake na Vyombo vya Habari Jijini Dodoma ambapo amesema miradi mingine iliyotekelezwa na serikali ya sweden inahusisha katika ujenzi wa bwawa la Mtera, bwawa la Kidatu.
Amesema kuwa serikali imekuwa na ushirikiano na nchi ya Sweden kwenye utekelezaji wa miradi ya umeme nchini ambapo wamekamilisha na kufunga mradi wa Makambako-Songea kupitia Njombe-Madaba wa Kilovoti 220 uliogharimu Sh. Bilioni 154.
Alisema mradi huo ulikuwa ukifadhiliwa na nchi hiyo owa asilimia 100 ambao ulizinduliwa mwaka 2017 ambao umeweza kuinufaisha wananchi 120.
“Kwa sasa nchi hiyo imebakiza ufadhili wake katika maswala ya Umeme ni umeme wa Hale ambapo wanafanyia matengenezo makubwa , alibainisha kwamba umeme wa hale ulianza kutumika tangu mwaka 1964 sasa Sweden inakalabati ili uweze kutumika vyema kwa mikoa ya jirani na Tanga., eo hii mradi huu unafungwa rasmi,”alisema
Mhandisi Mramba amesema kuwa kwamba nchi hiyo imefadhili Tanzania kwa miradi mingi ya nishati ya umeme nchi hiyo imehusika sana na umeme vijijini (REA) karibu nchi nzima kusambaza.
Hata hivyo amesema nchi hiyo pia imehusika kwa kiasi kikubwa katika utekelezaji wa mradi wa umeme kwa bwawa la Mtela na mikoa mingine ambayo imeweza kupatiwa miradi ya umeme wa jua (Sola).
Amesema kwa sasa Tanzania pitia Sweden ambayo imeendelea sana katika uzalishaji wa umeme.wa maji, imebaki kusaidia nchi katika ukarabati wa umeme wa hale ambako nako kunafanyiwa matengenezo makubwa ili tuzidi kunufaika na umeme huo wa maji.
Kwa upande wake Balozi wa Swedeni Mhe. Charlotta Ozaki Macias amesema mradi huu ulianza miaka 20 iliyopita nakuchukua takribani miaka 17 kukamilisha kutokana na ukubwa wa kazi yenyewe.
“Tumefanya kazi na Shirika la Umeme Tanesco na Wakala wa Usambazaji wa Umeme Vijijini (REA) na niwashukuru wadau wote waliohusika katika ujenzi wa miradi hii kwa kusaidia maelfu ya wananchi kupata huduma ya nishati ya umeme,” alisema Mhe. Balozi.
Huu ni Ushuhuda mzuri wa ushirikiano uliopo kati ya serikali ya Tanzania na Sweeden kwa sababu upatikanaji wa nishati ya umeme ni hitaji la msingi kwa jamii.
Ikumbukwe kwamba Mradi wa Umeme Makambako hadi Songea ulizinduliwa na aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Mgaufuli Mwaka (2017) na Ulikuwa Mkopo Serikali ya Sweeden na leo ilikuwa tukio la kuhitimisha na kufanga mradi.