Mkurugenzi wa mipango,Sera na Utafiti Zanzibar ,Issa Sarboko Makarani akizungumza kwenye kongano hilo mkoani.Arusha
Happy Lazaro,Arusha .
MAAFISA Rasilimali watu na utawala kutoka nchi mbalimbali barani Afrika wamekutana mkoani Arusha kwa lengo la kupewa uelewa kuhusu matumizi ya digitali katika kurahisisha utendaji kazi wao .
Aidha kongamano hilo limeandaliwa na THRAPA huku maafisa hao wakitakiwa kutumia mifumo ya sasa ya kazi kwa kuzingatia misingi ya kidigitali ili kurahisisha utendaji wao na hivyo kuondokana na mfumo wa zamani wa kutumia karatasi kujaza taarifa ambao hauna tija .
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa mipango,Sera na Utafiti Zanzibar ,Issa Sarboko Makarani kwa niaba ya Waziri wa ujenzi mawasiliano na uchukuzi Zanzibar wakati akifungua kongamano la kimataifa juu ya maswala ya kidigitali katika maeneo ya kazi .
Amesema kuwa mifumo ya utendaji kazi Ulimwengu imebadilika na mazingira ya kazi nayo yamebadilika hivyo maafisa hao hawana budi kuhakikisha wanatumia mfumo wa kidigitali Ili kurahisisha utendaji wao
Makarani,amesema kutokana na mabadiliko ya teknolojia Ulimwenguni ,Serikali imeamua kuendesha mafunzo hayo kwa maafisa hao ili kuwajengea uwezo na uelewa waweze kufanya kazi zao kwa kuzingatia misingi ya kidigitali na kuonfokana na mfumo wa zamani ambao hauna ufanisi mkubwa.
Amesema mabadiliko hayo ya teknolojia yamepelekea maafisa hao kupewa mafunzo hayo ili kuwa tayari kufanya kazi kisasa ili kupata matokeo mazuri katika kazi kwa kurudisha mfumo wa digitali na kuwawezesha kuboreshe utendaji wao.
“hayo ni kuwatayarisha wafanyakazi wa Sekta za umma Nchini kufanya kazi katika misingi ya kidijitali kutokana na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia inauokuwa kila kukucha.”amesema .
Makarani ameongeza kuwa, mfumo wa sasa wa kidigitali hauna nafasi ya mtu kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wafanye kazi kisasa kwa kutumia mitandao ambayo inarahidisha utendaji kazi na kuleta ufanisi na matokeo yenye manufaa.
Naye Mwenyekiti wa Taasisi ya Wataalamu wa Rasilimali watu na utawala Tanzania (THRAPA) Christopher Kabalika Mwansasu,
amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwakusanya mameneja raslimali watu Ili kuwapa Elimu ya matumizi ya kidigitali pahali pa kazi .
Ametaja nchi zilizoshiriki kuwa ni pamoja.na Afrika kusini,Ghana,Ethiopia, Uganda,Kenya,Rwanda,Zanzibar,na Tanzania .
Amesema Ulimwengu umebadilika Sasa mambo mengi yapo kwenye teknolojia hivyo maafisa hao ndio wanaoleta chachu ya utendaji kazi lazima wapewe Elimu hiyo ili kuwajengea uelewa wa matumizi ya kidigitali sehemu za kazi na kufungua wigo wa uchumi wa bluu Nchini.
Mwansasu,amesema Programu hizo zina faida kubwa hivyo wanao wajibu wa kuwaletea Watanzania vitu mbalimbali ili kuhakikisha utendaji wa kutumia kidigitali unapewa kipaumbele.
Ameongeza kuwa mfumo huo unawaunganisha maafisa hai na wenzao ili wawe na mawasiliano ya pamoja pia Viongozi wanaweza kufanya maamuzi bila kuwepo ofisini kutokana na matumizi ya mifumo ya kidigitali inarahidisha utendaji kazi.na mafunzo hayo yataleta mabadiliko kwenye Utumishi wa umma kuelewa umuhimu wa matumizi ya mfumo wa kisasa wa digital pahali pa kazi ili waweze kuboresha utendaji wao.
Amesema Programu mbalimbali za matumizi ya mfumo wa digitali na matumizi ya akili mnemba, zinafundishwa Kwa kuwa teknolojia inakuwa hivyo kuleta chachu kwenye utendaji wao.
Amefafanua kuwa, matumizi ya mifumo unarahisisha kuwepo mtiririko kwenye maeneo mbalimbali ya kazi na hivyo kufungua uchumi hivyo maafisa Utumishi hao lazima watambue kwamba mfumo wa digital inakuwa ni kipaumbele Kwa kuwa unamwezesha kufanya maamuzi bila kuwepo ofisini.
Afisa Utumishi mwandamizi kutoka mfuko wa pembejeo ,Basuta Milanzi,amesema kuwa Dunia ipo kwenye mfumo wa dojitali na bila mfumo hakuna kinachoweza kufanyika hivyo mafunzo hayo ni muhimu kwa kuwa yanaelejeza na kusisitiza matumizi ya mfumo wa dogijitali.
Ameongeza kuwa,kwa sasa kuna mifumo mingi inayotumika kurahisisha utendaji kazi tofauti na zamani walikuwa wakitumia karatadi kujaza OPRAS ili kupima utendaji wa mtumishi,lakini Sasa wanatumia mfumo kujaza na mfumo umerahisisha utendaji.

Mkurugenzi wa mipango,Sera na Utafiti Zanzibar ,Issa Sarboko Makarani akizungumza kwenye kongano hilo mkoani.Arusha .

Mwenyekiti wa Taasisi ya Wataalamu wa Rasilimali watu na utawala Tanzania (THRAPA) Christopher Kabalika Mwansasu akizungumza na waandishi wa habari kwenye kongamano hilo.

Washiriki mbalimbali wa kongamano hilo wakisikiliza mada mbalimbali mkoani Arusha