Waananchi wa Kitongoji cha Hawiga Kijiji cha Shaji Kata ya Mlangali wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe wametakiwa kuacha tabia ya kuwahusisha wazee wa Kitongoji hicho na imani za kishirikina kwa kuwa vitendo hivyo hupelekea kutendewa vitendo vya ukatili na kusababisha ulemavu wa kudumu na vifo.
Kauli hiyo ilitolewa Februari 27, 2025 na Polisi Kata ya Mlangali Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Robart Kasunga wakati akitoa elimu kwa wananchi hao juu ya umuhimu wa kuwatunza na kuwalea wazee kwani kundi hilo kwa sasa ni hazina kubwa katika malezi bora ya jamii ya sasa.
“Acheni kuwahusisha wazee au watu wa makamu moja kwa moja na imani za kishirikina kufanya hivyo ni kosa kisheria na atakayebainika kufanya hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo” alisema Mkaguzi Kasunga.
ReplyReply to allForward |