Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe Februari 27, 2025 limefanya doria katika Wilaya zote nne, Mbozi, Songwe, Ileje pamoja na Momba kwa lengo la kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao, zoezi hilo limeongozwa na Mkuu wa Operesheni Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Nicholas Livingstone na kusema kwamba Mkoa wa Songwe uko salama, na amewataka wananchi kuendelea na shughuli zao za kiuchumi bila hofu wala mashaka yoyote kwani doria hizo ni endelevu na zinalenga kukabiliana na uhalifu na wavunjifu wa amani katika Nchi yetu.
PICHA NA ISSA MWADANGALA